Katika kusherekea sikukuu ya wanawake duniani Machi 8, wafanyakazi wanawake wa migodi ya dhahabu ya Acacia ya Buzwagi na Bulyanhulu wametembelea wodi ya wazazi na wodi ya watoto wenye mahitaji maalum katika hospitali ya Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga na kutoa msaada/zawadi ya bidhaa mbalimbali yakiwemo maziwa kwa ajili ya watoto wenye mahitaji maalum, vitenge, nguo za watoto, mafuta ya watoto, sabuni n.k. Picha zote na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Acacia Buzwagi & Bulyanhulu
Wafanyakazi wanawake wa migodi ya dhahabu ya Acacia ya Buzwagi na Bulyanhulu wakiwa na bidhaa mbalimbali kabla ya kukabidhi kwenye wodi ya wazazi na wodi ya watoto wenye mahitaji maalum katika hospitali ya Wilaya ya Kahama.
Wafanyakazi wanawake wa migodi ya dhahabu ya Acacia ya Buzwagi na Bulyanhulu wakimpatia zawadi mwanamke mwenzao katika wodi ya wazazi na wodi ya watoto wenye mahitaji maalum katika hospitali ya Wilaya ya Kahama leo Machi 8,2019.
Wafanyakazi wanawake wa migodi ya dhahabu ya Acacia ya Buzwagi na Bulyanhulu wakiwa wamebeba mtoto
Wafanyakazi wanawake wa migodi ya dhahabu ya Acacia ya Buzwagi na Bulyanhulu wakiendelea kutoa msaada katika hospitali ya Wilaya ya Kahama
Social Plugin