Wafanyakazi wa kampuni ya mawasiliano ya Zantel walipo Dar es Salaam na Zanzibar wameshiriki kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani kwa kufurahi pamoja na kusikiliza mada za kuwatia moyo, kuwajengea uwezo na jinsi ya kukabiliana na changamoto mbalimbali za kikazi na katika maisha yao ya kila siku nje ya kazi.
Hafla za kuadhimisha siku hiyo muhimu iliyoandaliwa na kampuni ya Zantel ilifanyika katika hoteli ya Epidol Masaki jijini Dar es Salaam na hoteli ya Golden Tulip iliyopo Zanzibar.
Mfanyakazi wa Zantel akichangia mawazo baada ya kusikiliza mada zilizotolewa.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Zantel , wakiwa katika Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika katika hoteli ya Epidol Masaki jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa Zantel wakiwa katika picha ya pamoja katika hoteli ya Epidol.
Wafanyakazi wa Zantel Zanzibar wakiwa katika picha ya pamoja baada ya maadhimisho hayo.
Social Plugin