Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ATEMBEZEWA KICHAPO BAADA YA KUNASWA AKIIBA NGUO ZA MAREHEMU MOCHWARI


 Kizazaa cha aina yake kimeshuhudiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kakamega nchini  Kenya baada ya mwanaume mmoja kufumaniwa na kupewa kichapo cha mbwa msikitini kwa tuhuma ya kuiba nguo za marehemu. 

Tukio hilo limetokea Alhamisi, Machi 29,2019 ambapo Mwanamume aitwaye Bastanik Wande kutoka kijiji cha Indangalasia alifumaniwa na ndugu wa marehemu akiiba nguo za marehemu katika chumba cha kuhifadhia maiti mjini humo.
Inaelezwa kuwa mshukiwa huyo ambaye ni jamaa wa karibu wa marehemu huenda alishirikiana na watu wasiojulikana kupanga njama ya kumuua ndunguye kwa njia tatanishi. 

Inadaiwa familia ilifanya tambiko ili kuwatesa wauaji na katika kujikinga kutokana na nuksi za aina yoyote ambazo huenda zikamwandama, hivyo Wande aliamua kuiba suti ya marehemu. 

Aidha familia ya marehemu ilikuwa imechukua hatua ya kumtenga mshukiwa katika mipango ya mazishi na walimwonya dhidi ya kugusa kitu chochote cha marehemu. 

"Tunashangaa kama anadai hakuhusika na kifo hicho basi mbona alikuwa akichukua nguo zake? Tulimwonya dhidi ya kuchukua mali yoyote ya marehemu na tumejitolea kusimamamia gharama zote za mazishi bila usaidizi wake, " alisema mmoja wa watu wa familia hiyo.

 Lakini Wande aliyakana madai hayo na kutaka mashirika ya kutetea haki za binadamu pamoja na serikali kuingililia kati na kumnasua kutoka kwa mtego huo.

 "Watu wamenivamia na kuniumiza, nilikuwa nimeenda mochwari kumtoa ndugu yangu na nimeshtuka kuwaona watu wamenizingira na wakaanza kunipiga na kuniumiza, naiomba serikali kuingililia kati na kunisaidia kwani nahisi watu hao wana nia mbaya kwa sababu wametishia kuzichoma nyumba pamoja na mali zote za marehemu." Wande alisema huku akiwa na maumivu mengi. 

Haijabainika kisa hicho kiliishia wapi ila vurugu hilo liliendelea kwa muda kabla ya kila mtu kwenda zake na kuuacha mwili wa marehemu.

 Hadi habari hii ikiandikwa, hamna ripoti kamili kutoka kwa familia ya marehemu kuhusu mipango baada ya kisa hicho kilichowashtua wengi katika hospitali hiyo. 
Chanzo -  Tuko

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com