Timu ya Yanga SC imeendelea kuwapa raha mashabiki wake baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Alliance FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.
Ushindi huo unaifanya Yanga SC ifikishe pointi 64 baada ya kucheza mechi 26, ikiendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi 11 zaidi ya Azam FC wanaofuatia kwenye nafasi ya pili, wakati mabingwa watetezi SImba SC wapo nafasi ya tatu kwa pointi zao 48 za mechi 19.
Haukuwa ushindi mwepesi, kwani pamoja na kucheza vizuri wakimiliki zaidi mpira, lakini Yanga SC walilazimika kusubiri hadi dakika ya 74 kupata bao leo pekee la ushindi.
Bao hilo limefungwa mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Amissi Joselyn Tambwe dakika 10 na ushei baada ya kuingia akitokea benchi kuchukua nafasi ya kiungo mkongwe wa kimataifa wa Tanzania, Haruna Moshi Shaaban ‘Boban’.
Social Plugin