Bao pekee la Haruna Shamte mnamo dakika ya 19 limeinyima alama tatu muhimu Yanga kwa kuipa ushindi Lipuli FC wa bao 1-0.
Mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Samora mjini Iringa umemalizika kwa matokeo hayo ambayo yamekuwa na machungu kwa wadau na mashabiki wa Yanga.
Yanga imepoteza mechi huku Kocha wake Mkuu, Mwinyi Zahera akiwa jijini Dar es Salaam baada ya kusema anataka kusafiri kuelekea Congo kwa ajili ya majukumu ya timu ya Taifa.
Matokeo haya yaifanya Yanga kusalia kwenye nafasi ya kwanza ikiwa na alama zake 67 huku Lipuli wakifikisha alama 44 kwenye nafasi ya nne.
Social Plugin