MBUNGE wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe ameichambua ripoti ya Mkaguzi na mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG, Progesa Mussa Assad aliyoitoa hivi karibuni ambapo pamoja na mambo mengine amesema kuwa katika taarifa hiyo amebaini kuwa Bajeti inayopitishiwa na Bunge sio Bajeti halisi.
Leo Jumapili Aprili 14, 2019 wakati akifanya uchambuzi wa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2017/18, Zitto amesema makusanyo yetu ya kodi bado ni kidogo (tax yield) na Tanzania ni ya mwisho katika nchi za Afrika Mashariki, uwiano wa makusanyo ukiwa ni 12% tu ya Pato la Taifa.
"Kwa Upande wa TRA Bado kuna changamoto kubwa ambazo zinahitaji kutatuliwa. Makusanyo yetu ya kodi Bado ni kidogo sana (tax yield) tukiwa wa mwisho Katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, uwiano wa makusanyo ukiwa ni 12% tu ya Pato la Taifa.
"Hii inatokana tax base kuwa ndogo na mifumo sio rafiki kwa walipa kodi. Inawezekana TRA huchukua Fedha za Taasisi kupeleka Hazina ili kuonyesha makusanyo zaidi ilhali hali sio hiyo.
"Serikali inapaswa kukaa na sekta Binafsi kujadili kwa unyoofu (honestly) njia bora ya kupanua wigo wa Kodi ili nchi iweze kujitegemea. "Amesema Zitto Kabwe
Zitto ameendelea kusema; "Kwenye bajeti ya mwaka wa fedha wa 2016/17, ambayo ni bajeti ya kwanza ya Serikali ya Awamu ya Tano, mipango ya Serikali ilikuwa ni kukusanya shilingi 29.5 trilioni, kwa mujibu wa ripoti ya CAG ya 2016/17, kati ya fedha hizo, Serikali ilikusanya shilingi 25.3 trilioni. Na hivyo, kutokufikia lengo la makusanyo kwa 14.33%. Kwenye uchambuzi wetu wa mwaka jana tulieleza kuwa bajeti za Serikali si halisia.
Social Plugin