Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Picha : AGAPE YAENDELEA KUTOA ELIMU YA KUKOMESHA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WASICHANA KWENYE MASOKO SHINYANGA

Meneja Miradi wa Shirika la Agape ACP, Mustapha Isabuda akitoa elimu ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na wasichana wafanyabiashara katika soko la Ibinzamata Mjini Shinyanga leo- Picha na Kadama Malunde - Malunde1 blog.

Wananchi katika Manispaa ya Shinyanga wameendelea kunufaika kwa elimu ya kutambua haki za binadamu ili kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na wasichana wafanyabiashara katika masoko inayotolewa na Shirika la Agape ACP. 

Leo Jumapili Aprili 14,2019 ilikuwa ni zamu ya Soko la Ibinzamata Mjini Shinyanga ambapo maafisa kutoka shirika la Agape ACP na Dawati la Jinsia na Watoto la Jeshi la polisi Shinyanga. 

Huo ni mwendelezo wa utoaji elimu ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake na wasichana wafanyabiashara kwenye masoko mbalimbali ikiwa ni utekelezaji wa mradi “Mpe Riziki Si Matusi” unaofadhiliwa na shirika la UN WOMEN kupitia Shirika la kitaifa la Equality for Growth (EfG). 

Afisa kutoka Dawati la Jinsia na Watoto jeshi la polisi wilaya ya Shinyanga, Secilia Kizza ametumia fursa hiyo kuitaka jamii kuachana na tabia ya kuwafanyia ukatili wanawake na wasichana wanaofanya biashara zao kwenye masoko kwa kuwadhulumu na hata kuwatolea lugha mbaya. 

“Toeni taarifa za matukio ya vitendo vya ukatili mahali sahihi, toeni kwa viongozi wenu wa masoko,viongozi wa serikali na pia katika jeshi la polisi kupitia dawati la jinsia na watoto”,alisema. 

Aidha aliwataka wananchi kuondokana na kasumba kuwa dawati la jinsia na watoto ni kwa ajili ya wanawake tu bali ni kwa ajili ya watu wote huku akiwahamasisha pia wanaume wanaofanyiwa ukatili kutoa taarifa katika dawati hilo ili wasaidiwe. 

Afisa Mradi wa “Mpe Riziki Si Matusi”, Helena Daudi aliwataka wanawake na wasichana wafanyabiashara kwenye masoko kutofumbia macho vitendo vya ukatili na kuwahamasisha kuvunja ukimya ili kukomesha ukatili katika masoko na hata kwenye familia zao.

Naye,Meneja Miradi wa Shirika la Agape ACP,Mustapha Isabuda alisema kukosekana kwa uaminifu katika ndoa imekuwa chanzo cha vitendo vya ukatili katika familia hivyo kuwaomba wanandoa kupendana na wanaume kuwahudumia wake zao badala ya kutamani wanawake wengine.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Afisa kutoka Dawati la Jinsia na Watoto jeshi la polisi wilaya ya Shinyanga, Secilia Kizza akitoa elimu namna ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na wasichana wafanyabiashara katika soko la Ibinzamata Mjini Shinyanga leo Jumapili Aprili 14,2019 - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Wakazi wa Ibinzamata wakimsikiliza Afisa kutoka Dawati la Jinsia na Watoto jeshi la polisi wilaya ya Shinyanga, Secilia Kizza. 
Afisa kutoka Dawati la Jinsia na Watoto jeshi la polisi wilaya ya Shinyanga, Secilia Kizza akiwasisitiza watu wanaofanyiwa vitendo vya ukatili kutoa taarifa mahali sahihi ikiwemo jeshi la polisi.
Wakazi wa Ibinzamata wakiwa eneo la tukio ambapo Chiza aliwahamasisha pia wanaume wanaofanyiwa ukatili katika familia zao waripoti katika dawati la jinsia na watoto ili wasaidiwe.
Afisa Mradi wa “Mpe Riziki Si Matusi” , Helena Daudi akiwahamasisha wanawake na wasichana kuvunja ukimya ili kukomesha vitendo vya ukatili kwenye masoko na hata katika familia zao.
Afisa Mradi wa “Mpe Riziki Si Matusi”, Helena Daudi akiendelea kutoa elimu kuhusu haki za binadamu.
Meneja Miradi wa Shirika la Agape ACP,Mustapha Isabuda akitoa elimu kuhusu haki za binadamu na kuitaka jamii kuacha kudhulumu akina mama wanaofanya biashara kwenye masoko wakiwemo Mama Lishe.
Wakazi wa Ibinzamata wakimsikiliza Meneja Miradi wa Shirika la Agape ACP,Mustapha Isabuda aliyetaka wanaume kuacha kuonea wanawake na wasichana kwenye masoko kwa kuwadhulumu na kuwashika shika bila ridhaa yao. 
Meneja Miradi wa Shirika la Agape ACP,Mustapha Isabuda akiwasisitiza wanaume kuacha kutamani watoto wa shule na kama wanapenda sana wanafunzi basi wawashonee sketi wake zao,huku akibainisha kuwa ukikamatwa umefanya mapenzi au umempa ujauzito mwanafunzi unatupwa jela miaka 30 kwa mujibu wa sheria.
Wananchi wakimsikiliza Isabuda.
Mwanasheria kutoka shirika la Agape CP, Suzana Musa (kulia) akigawa vipeperushi vinavyotoa elimu ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na wasichana kwenye masoko.
Wananchi wakisoma na kuomba vipeperushi vinavyotoa elimu ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na wasichana kwenye masoko baada ya kupewa na Afisa kutoka Shirika la Agape ACP,Kitengo cha Miradi,Teresia Venant (kulia). 
Vijana kutoka kundi la Shinyanga Arts Group linaloongozwa na Msanii Chapchap wakitoa burudani wakati elimu ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na wasichana kwenye soko la Ibinzamata ikiendelea.
Msanii Chapchap akitoa burudani ya kucheza muziki.
Wananchi wakifurahia burudani kutoka kwa Msanii Chapchap.
Mzuka ukampanda Mama huyu...,akaamua kuingia kati ya kuonesha maufundi ya kucheza pamoja na Msanii Chapchap.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com