Washukiwa wa uhalifu wameripotiwa kudukua mashine ya ATM ya benki ya Barclays na kuiba KSh 11 milioni Jumapili Aprili 21,2019 wakati walimwengu wakisherehekea sikukuu ya pasaka.
Machine hayo ya ATM ni ya benki ya Barclays ya tawi la South B, ile iko Kenyattta National Hospital na ya mtaa wa Buru buru.
Kulingana na uchunguzi wa polisi, wizi huo ulitekelezwa na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo.
Afisa mmoja wa G4S alisema KSh 7 milioni ziliwekwa kwenye mashine hizo Aprili 18,2019 na baadaye KSh 6.2 milioni zilipotea huku ikidaiwa mashine haikuwa ikifanya kazi. Uchunguzi umeanzishwa kufuatia uhalifu huo.
Social Plugin