Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BENKI YA CRDB NA UBA YAIDHAMINI SERIKALI UJENZI WA STIEGLERS GEORGE


Benki ya CRDB kwa kushirikiana na benki ya UBA zimetoa Dola za Kimarekani milioni 737.5 ambazo ni sawa na Sh Trilioni 1.7 kwa ajili ya kuidhamini serikali katika ujenzi wa mradi wa umeme wa Rufiji wa Stieglers George.


Akizungumza katika uzinduzi huo jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa benki ya UBA, Usman Isiaka alisema fedha hizo ni dhamana ya benki inayotakiwa na mkandarasi katika mradi huo ambao utagharimu Sh trilioni 6.6.

“Kwa mujibu wa masharti ya mkataba huo, umoja huo unahitajika kutoa dhamana za benki za kigeni na za ndani zikiwa ni jumla ya Dola za Kimarekani milioni 737.5 kupitia utekelezaji wa mradi na dhamana ya malipo ya awali kwa mradi huo.

“Kwa kuanzia, Benki ya CRDB na UBA zimeshirikiana na Benki ya Afrika Export-Import (Afrieximbank) na benki nyingine za Misri kutoa dhamana za benki kwa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) ambapo sehemu ya dhamana hizo tumezitoa hapa leo (jana),”alisema Isiaka.

Mradi  huo mkubwa unatarajia kuiongezea nguvu Serikali kukabiliana na upungufu wa umeme kwa kuwa uchumi wa nchi na idadi ya watu inaongezeka.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com