Mkufunzi kutoka Mradi wa Boresha Habari ukiendeshwa chini ya uratibu wa mashirika yasiyo ya Kiserikali ya Internews na FHI 360 unaofadhiliwa na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID),Temigunga Mahondo wakati akitoa elimu kwa waandishi wa habari wa kituo cha redio Nuru Fm Iringa juu ya kusaidia kupaza sauti za wanyonge kupitia kalamu zao, hususani wale ambao wanaishi maeneo ya vijijini.
Mkufunzi kutoka Mradi wa Boresha Habari ukiendeshwa chini ya uratibu wa mashirika yasiyo ya Kiserikali ya Internews na FHI 360 unaofadhiliwa na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID),Temigunga Mahondo akiwaeleza waandishi wa habari wa kituo cha redio Nuru Fm Iringa juu ya kusaidia kupaza sauti za wanyonge kupitia kalamu zao, hususani wale ambao wanaishi maeneo ya vijijini.
Baadhi ya waandishi wa habari wa kituo cha redio Nuru Fm Iringa wakimsikiliza mkufunzi kutoka Mradi wa Boresha Habari ukiendeshwa chini ya uratibu wa mashirika yasiyo ya Kiserikali ya Internews na FHI 360 unaofadhiliwa na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID),Temigunga Mahondo wakati akitoa elimu kwa juu ya kusaidia kupaza sauti za wanyonge kupitia kalamu zao, hususani wale ambao wanaishi maeneo ya vijijini.
***
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
Waandishi wa habari wa kituo cha redio Nuru fm 93.5 mkoani Iringa wametakiwa kujikita kuandika habari za uchunguzi kwa kuibua matatizo ndani ya jamii, ambayo yamekuwa yakifichika na kutopaziwa sauti, jambo ambalo litawasaidia wananchi kutatulia kero ambazo zimekuwa zikiwakabili sababu ya kukosa sehemu pa kuzisemea.
Hayo yamebainishwa na mkufunzi kutoka Mradi wa Boresha Habari ukiendeshwa chini ya uratibu wa mashirika yasiyo ya Kiserikali ya Internews na FHI 360 unaofadhiliwa na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID),Temigunga Mahondo wakati akitoa elimu kwa waandishi wa habari wa kituo cha redio Nuru Fm Iringa juu ya kusaidia kupaza sauti za wanyonge kupitia kalamu zao, hususani wale ambao wanaishi maeneo ya vijijini.
Alisema waandishi wa habari wanamsaada mkubwa sana ndani ya jamii kwa kupaza sauti za wanyonge kupitia kalamu zao, kwa kuibua matatizo ambayo yamekuwa yakiwakabili wananchi, na hasa kwa kuandika habari za uchunguzi ili jamii ipate kutatuliwa kero zao.
“Naombeni waandishi wa habari mjikite zaidi kuandika habari za uchunguzi kwa kuibua matatizo ambayo yamekuwa yakijificha ndani ya jamii, hususani kwa wale wananchi wanaoishi maeneo ya vijijini, ambao wamekuwa wakikosa wa kuwapazia sauti na kuendelea kuishi maisha ya shida,”AlisemaMahondo
Mahondo alisema kuwa waandishi wa habari mkijikita kwenye habari hizi mtakuwa mnaisaidia jamii ya wananchi wale wale wanyonge kwa kuwa tayari mtakuwa ninyi ndio sauti yao kwa kipindi chote ambacho mtakuwa mnaandika habari hiz.
“Kuandika habari hizi zinanafasisi kubwa wa kuzifanya kwa kuangalia changamoto na manufaa katika sekta ya Afya,sekta elimu,sekta ya miundombi,sekta ya kilimo na mazingira na utapata uwanda mpana sana wa kufanya habari zenye tija kwa jamii” alisema Mahondo
Aidha Mahondo alisema,licha ya jamii kuhitaji kupata habari za kiburudani ambazo zimekuwa zikiwaburudisha kwa muda mfupi tu lakini kubwa zile habari ambazo zinasaidia kutatua changamoto za wananchi ndio zinatija hasa kwenye jamii kwa kufanikisha kutatua matatizo yao.
“Hakuna wananchi ambaye hapendi kupata burudani hivyo tunaangalia aina gani ya burudani ambayo inawapa zaidi furaha jamii kwa kipindi kirefu ambayo itawasaidia kufanya shughuli za kimaendeleo ambazo zitawaletea faida wananchi” alisema Mahondo
Naye mwaandishi wa habari na mtangazaji wa kipindi cha Sunrise Power cha Nuru fm Godfrey Mengele aliwatupia lawama wananchi hususani wa maeneo ya vijijini, ambapo wamekuwa waoga kutoa ushirikiano kwa waandishi wa habari kwa kushindwa kuzungumza matatizo yanayowakabili.
alisema kuwa waandishi wa habari hawezi kuchunguza habari bila ya kupewa taarifa (Tipu) juu ya tatizo linalo wakabili wananchi, pamoja na kutozungumza na wahusika waliofanyiwa matukio hayo ya ukatili ama ndugu, ambapo wananchi hao hua hawapo tayari kuzungumza na kuwakimbia waandishi.
Mengele aliwataka wananchi kuachana na tabia za uoga pale wanapotaka kusemewa matatizo yanayo wakabili kupitia vyombo vya habari, bali wawe karibu na media ambazo ndio msaada mkubwa kwao.
“Wananchi wamekuwa waoga sana kutupa habari ambazo zinawagusa wao kwa kuhofia kufikishwa polisi,kwenye ofisi za serikali za mitaa hata mahakamani kutoa ushaidi ndio maana waandishi tunapata wakati mgumu pia kuandika habari hizi” alisema Mengele
Lakini alitoa rai kwa waandishi wa habari kujikita kuandika habari za kichunguzi ambazo ndio zimekuwa zikiibua matatizo ya wananchi na kutafutia ufumbuzi wa kutatua changamoto zao.
Kwa upande wake mtangazaji wa kipindi Street Bamiza Roger Magoha alisema mafunzo aliyopata yatamsaidia kukuza vipaji halisi vya wasanii wanaopenda kutoa burudani na kujua aina gani ya burudani wasikilizaji wanapenda kusikiliza.
“Sasa nitafanya uchunguzi kujua wasikilizaji wangu wanapenda aina gani ya burudani kwa kuwa nimeshapata mbinu za kufanya uchuzi huo kutoka kwa mkufunzi wa Mradi wa Boresha Habari ukiendeshwa chini ya uratibu wa mashirika yasiyo ya Kiserikali ya Internews na FHI 360 unaofadhiliwa na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID),Temigunga Mahondo” alisema Magoha
Magoha aliongeza kwa kusema kuwa amejifunza kufanya mahojiano bora na wasanii mbalimbali pamoja na viongozi hivyo mafunzo hayo yamemwogezea kitu kipya kichwani mwake ambacho hapo awali hakuwa nacho.
Tarehe 17 Januari 2018, Serikali ya Marekani kwa kupitia Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID), ilizindua mradi wa kuimarisha asasi za kiraia na vyombo vya habari uitwao Boresha Habari Katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam, mradi huo ukiendeshwa chini ya uratibu wa mashirika yasiyo ya Kiserikali ya Internews na FHI 360, mradi wa Boresha Habari utashirikiana na wabia wa Kitanzania, ikiwa ni pamoja na: Baraza la Habari Tanzania, Tanzania Bora Initiative, na Jamii Media; ili kuboresha weledi miongoni mwa waandishi wa habari na kusaidia kuweka mazingira yaliyo wazi kwa vyombo vya habari.
“Serikali ya Marekani imedhamiria kwa dhati kusaidia kuinua ujuzi na weledi wa vyombo vya habari na asasi zisizo za kiserikali za Kitanzania hususan katika kuwawezesha wanawake na vijana kupaza sauti zao na kueleza dukuduku zao kwa ufanisi,”
Katika kipindi cha miaka mitano ijayo, mradi wa Boresha Habari unalenga kufanya kazi na wadau wa vyombo vya habari katika mikoa ya Dar es Salaam, Zanzibar, Iringa, Mbeya, Morogoro, Arusha, Manyara, Dodoma, Tanga, Mtwara, Mwanza na Kigoma.
Aidha, mradi wa Boresha Habari utatoa mafunzo na msaada wa kitaalamu kwa vyombo vya habari vya humu nchini ukivisaidia kuanza kutumia teknolojia za kidijitali na kuimarisha uwezo wao wa kiusimamizi na kifedha.
Hali kadhalika, mradi huu utatoa mafunzo kwa asasi za kiraia ili ziweze kushirikiana vyema na vyombo vya habari katika kusukuma mbele jitihada zao. Kwa kuzingatia umuhimu wa redio za jamii kama vyanzo maarufu vya habari za maeneo husika, mradi wa Boresha Habari utafanya kazi na vituo mbalimbali vya redio nchini kote ili kuboresha uwezo wao wa kitaalamu na uendelevu katika masuala ya kifedha.
Kwa taarifa zaidi, tafadhali wasiliana na Ofisi ya Habari ya Ubalozi wa Marekani Dar es Salaam kwa simu namba: +255 22 229-4000 au kwa barua pepe: DPO@state.gov.
Social Plugin