HALIMA MDEE APIGWA ‘STOP’ BUNGENI KWA KUUNGA MKONO KAULI YA CAG


Bunge limeazimia kumfungia Mbunge wa Jimbo la Kawe, Halima Mdee kutohudhuria mikutano miwili baada ya kumkuta mwanasiasa huyo na hatia ya kuwa na dhamira ovu ya kukidhalilisha chombo hicho.

Taarifa iliyotolewa bungeni, Dodoma, leo Jumanne imesema kuwa Halima Mdee alikiri mbele ya Kamati yake ya Maadili, Haki, Kinga, Maadili na Madaraka ya chombo hicho kuwa aliunga mkono kauli ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuwa “Bunge ni dhaifu.”

Hii ni mara ya nne mbunge huyo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kupewa adhabu ya kufungiwa kuhudhuria Bunge.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم