Picha : NGOME YA CUF SHINYANGA MJINI YABOMOKA...VIONGOZI WOTE,WANACHAMA 200 WATIMKIA ACT WAZALENDO


Chama cha ACT- Wazalendo wilaya ya Shinyanga mjini kimevuna viongozi wote wa Chama cha wananchi CUF wilayani humo wakiwemo na wanachama 200, ambao wamedai kutokubaliana na maamuzi ya Mahakama ya kumpatia chama hicho Profesa Ibrahimu Lipumba pamoja na kuwa mwenyekiti Taifa ambaye aliwakimbia siku chache kabla ya uchaguzi mkuu 2015.


Walisema Profesa Ibrahimu Lipumba hafai kuwa kiongozi ikiwa aliwakimbia kwenye kipindi cha mapambano ya uchaguzi mkuu 2015 na kuonekana chama ni kidhaifu, ambapo tena mtu huyo huyo amekabidhiwa chama jambo ambalo hawajafurahishwa nalo na hivyo kuamua kuhamia upande wa pili ACT-Wazalendo.

Akizungumza siku ya Jumamosi Aprili 6,2019 Katibu wa Chama cha Wananchi CUF wilaya ya Shinyanga Mjini Said Juma Issa wakati wakihama chama hicho kwenda ACT-Wazalendo, alisema wameamua kundoka kwenye chama hicho kwa hiari yao wenyewe bila ya kushawishiwa na mtu.

“Baada ya Lipumba kukabidhiwa chama tena, sisi kama viongozi wa CUF Shinyanga Mjini tukiwa na kamati tendaji ya watu 12, tukaona hatuna haja tena ya kuendelea kupigania chama ambacho kinaongozwa na kiongozi ambaye siyo shupavu kwenye mapambano, ndipo tukaona ni bora tuhamie upande wa pili,” alisema Issa.

“Hivyo tunaomba Chama cha ACT-Wazalendo mtupokee sisi viongozi pamoja na wenzetu ambao wapo 200, na wengine wengi watazidi kuja ikiwa kwa leo wamepata udhuru, tushirikiane kwa pamoja katika mapambano ya kisiasa ili tupate kushika dola na kuwatumikia wananchi,”aliongeza.

Naye Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo wilaya ya Shinyanga Mjini Twaha Makani, aliwapokea wanachama hao wapya kutoka chama cha wananchi CUF, huku akiwataka wafuate misingi na katiba ya chama hicho, ili kukijenga chama ambacho kwa sasa ndiyo kinaaminiwa na watanzania kuwaletea ukombozi.

Kwa upande wake mjumbe wa mkutano mkuu wa chama hicho cha ACT-Wazalendo Nyangaki Shilungshela, aliwatahadharisha wanachama hao wapya kutokuwa na majungu na makundi, ambayo yamekuwa yakisababisha migogoro ndani ya chama na hatimaye kukosa uelekeo na kusambaratika.

TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI

Viongozi wa Chama cha wananchi CUF wilaya ya Shinyanga Mjini (kulia( wakikabidhi vitu vya Chama hicho zikiwemo na kadi 200 za wanachama wa CUF, wakati wakihamia rasmi ACT-Wazalendo.

Katibu wa Siasa, habari na uenezi kutoka Chama cha CUF (kulia) Omari Gindu akikabidhi Bendera za CUF kwa uongozi wa ACT-Wazalendo na kutokuwa viongozi tena kwa madai ya kutokubali kuongozwa na Profesa Ibrahimu Lipumba kuwa Mwenyekiti wao.

Katibu wa Siasa, habari na uenezi kutoka Chama cha CUF mkono wa kulia Omari Gindu akikabidhi kadi za wanachama wa CUF 200 na kuhamia rasmi ACT-Wazalendo.

Viongozi wa CUF wakiendelea kukabidhi vifaa kwa ACT-Wazalendo.

Zoezi la kukabidhi vifaa vya CUF likiendelea.

Katibu wa Chama cha wananchi CUF wilaya ya Shinyanga Mjini Said Juma Issa akizungumza kwa niaba ya wenzake 200 ambao wamekihama chama hicho na kuhamia chama cha ACT-Wazalendo.

Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo wilaya ya Shinyanga Mjini Twaha Makani akiwakaribisha wanachama wapya kutoka CUF na kuwataka wafuate misingi ya katiba ya chama hicho ili wapate kukijenga chama kwa pamoja na kupata ushindi wa kushika dola kwenye uchaguzi mkuu ujao pamoja na kupata viongozi wengine kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa Oktoba mwaka huu.

Katibu wa Chama cha ACT-Wazalendo mkoa wa Shinyanga Sebastian Tafuta akiwakaribisha wanachama hao wapya wa CUF kujiunga Rasmi na ACT-Wazalendo mahari ambapo ni salama na ndiyo chama pekee kinacho aminiwa na wananchi katika kuwaletea ukombozi.

Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo mkoa wa Shinyanga Siri Yasini, akizungumza wakati wa kupokea wanachama wapya kutoka CUF Nakubainisha kuwa wameongeza Jeshi la Mapambano kisiasa.

Katibu Mwenezi wa Chama cha ACT-Wazalendo mkoa wa Shinyanga Chrisant Msipi, akiwakaribisha wanachama hao kutoka CUF kuwa wawe wamoja kukijenga Chama.

Mjumbe wa Kamati kuu kutoka Chama cha ACT-Wazalendo Nyangaki Shilungushela, akiwatahadharisha wanachama hao wapya kutoka CUF kuacha majungu, na kutengeneza makundi ambayo ni chanzo cha migogoro ndani ya chama.

Viongozi na wanachama wa CUF wilaya ya Shinyanga Mjini wakisikiliza nasaha kutoka kwa viongozi wa ACT-Wazalendo wakati wakiwakaribisha rasmi kwenye chama hicho.

Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo mkoa wa Shinyanga Siri Yasini mkono wa kushoto akimkabidhi Kadi ya uanachama ya ACT-Wazalendo katibu wa CUF wilaya ya Shinyanga Mjini Said Juma Issa.

Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo mkoa wa Shinyanga Siri Yasini mkono wa kushoto akimkabidhi Kadi ya uanachama ya ACT-Wazalendo katibu wa Siasa, Habari na Uenezi CUF wilaya ya Shinyanga Mjini Omari Gindu.

Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo mkoa wa Shinyanga Siri Yasini akiendelea na zoezi la ugawaji kadi kwa wanachama wapya kutoka CUF waliojiunga na chama hicho.

Zoezi la ugawaji kadi likiendelea.

Zoezi la ugawaji kadi likiendelea.

Viongozi na wanachama kutoka CUF wakila kiapo cha kutii miongozo na Katiba ya Chama cha ACT-Wazalendo, mara baada ya kumaliza kujiunga rasmi na kukabidhiwa kadi za uanachama.

Na Marco Maduhu-Malunde 1 Blog.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post