Kaimu Mkurugenzi wa Biashara wa Vodacom, Linda Liwa (katikati) akiongea na wananchi waliojitokeza katika uzinduzi huo.
KAMPUNI ya Vodacom imezindua promosheni ya Data Datani inayompatia mteja Bonus za MB (Internet) hadi mara mbili ya bando kila anaponunua kifurushi cha Internet kwa bei ileile.
Uzinduzi huo umefanyika leo katika viwanja vya Mbagala-Zakhem jijini Dar es Salaam ukiongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Biashara wa Vodacom, Linda Liwa.
Bonus hizo za MB zinamwezeha mteja wa Vodacom kuangalia video kupitia Youtube, kuperuzi kwenye mitandao ya kijamii (WhatsApp, Facebook na Instagram).
Wateja wakijiunga na bando kujishindia simu za Smartphone.Liwa amesema wameanzisha promosheni ya ubunifu na kuwaelimisha wateja jinsi ya kutumia bando baada ya malalamiko mbalimbali kutoka kwa wateja kupoteza MB zao kutoka kwenye mtandao Supa wa Vodacom wa 4G na na kwamba hawana mpinzani kwenye promosheni hiyo ya Data Datani.
Katika hafla hiyo pia zimetolewa zawadi za simu aina ya Smartphone kwa wateja wa Vodacom waliokuwepo katika uzinduzi huo kwa kuwauliza maswali mbalimbali ya jinsi ya kujiunga na bando kutoka Vodacom.
Uzinduzi huo ulifanyika sambamba na burudani mbalimbali.
Kwa mujibu wa promosheni hiyo, fursa zilizopo ni pamoja na mtu kumnunulia rafiki yake vifurushi vya internet na kufurahia Bonus za Data Datani. Pia mteja anaweza kupata Bonus kwa kujiunga/kununua vifurushi vya internet kwa njia zifuatazo:
- Piga *149*01# chagua Internet>bando za internet/masaa 24, siku 7 au siku 30
- Piga *150*00# chagua nunua kifurushi/muda wa maongezi >Nunua vifurushi>internet/bando za internet
- My Vodacom App
- M-PESA APP
- Tovuti ya Vodacom (www.vodacom.co.tz)
Kwa Vodacom: Kila kitu ni mwendo wa kudata datani na Vodacom kwa kupata Bonus za MB hadi mara mbili ambapo mteja anachotakiwa ni kupiga *149*01# na kuchagua Intaneti na anunue kifurushi akipendacho ili kujipatia bonus papo hapo.
Social Plugin