Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Picha : RAIS MAGUFULI AZINDUA MJI WA SERIKALI DODOMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo mara baada ya kukata utepe kwenye jengo la Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora kuashiria uzinduzi wa Mji wa Serikali katika eneo la Mtumba leo jijini Dodoma. Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Balozi John Kijazi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, George Mkuchika, Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais Mstaafu, Mzee Samwel Malecela, Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli,Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Salma Kikwete, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Bashiru Ally.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akipongezana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na baadhi ya viongozi wengine mara baada ya kufunga jiwe la msingi kuashiria uzinduzi rasmi wa Mji wa Serikali katika eneo la Mtumba leo jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mji wa Serikali ulijengwa katika eneo la Mtumba jijini Dodoma leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia Mkuu wa Majeshi na Ulinzi, CDF, Venance Mabeyo akimbadilishia cheo kutoka Kanali hadi kuwa Brigedia Jenerali wa Jeshi la Wananchi Tanzania(JWTZ), Brigedia Jenerali Charles Mbuge wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mji wa Serikali ulijengwa katika eneo la Mtumba jijini Dodoma leo. Wengine wanaoshuhudia zoezi hilo ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Simon Sirro. Brigedia huyo amepewa cheo hicho na Mhe. Rais kufuatia uchapakazi wake katika kusimamia miradi ya ujenzi mbalimbali inayotekelezwa na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kwa kushirikiana na JKT. Baadhi ya wananchi na wabunge wakifuatila hafla ya uzinduzi wa Mji wa Serkali uliojengwa katika eneo la Mtumba jijini Dodo leo.Mkurugenzi wa Idara ya Habari - MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akiteta jambo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Adeladius Kilangi, Waziri wa Madini, Dotto Biteko, na Selemani Jaffo walipokutana katika hafla ya hafla ya uzinduzi wa Mji wa Serikali ulijengwa katika eneo la Mtumba jijini Dodoma leo.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kikosi Kazi kilichoratibu zoezi la Serikali Kuhania Dodoma mara baada ya uzinduzi wa Mji wa Serikali katika eneo la Mtumba leo jijini Dodoma.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya Mawaziri na Manaibu Waziri wa Wizara mbalimbali mara baada ya uzinduzi rasmi wa Mji wa Serikali katika eneo la Mtumba leo jijini Dodoma. .(Picha na Frank Shija - MAELEZO).

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com