Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

GODBLESS LEMA ASIMAMISHWA KUHUDURIA MIKUTANO MITATU YA BUNGE....WABUNGE WA UPINZANI WASUSA NA KUTOKA NJE


Bunge limepitisha Azimio la kumzuia  Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema kuhudhuria mikutano mitatu ya Bunge kwa kosa la kulidhalilisha Bunge kwa kusema “Bunge ni dhaifu” na alipoitwa kwenye kamati ya Bunge ya kinga haki na madaraka ya Bunge hakuonyesha kujutia kufanya kosa hilo.


Akiwasilisha hoja hiyo Bungeni leo April 4, 2019  mwenyekiti wa kamati hiyo Emmanuel Mwakasaka  amesema kuwa Mbunge huyo alipopewa nafasi ya kujitetea kwenye kamati alisema ahukumiwe tu kwani alichozungumza ni kweli.

Wakati azimio hilo linapitishwa wabunge wa Chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA  wamesusia kikao hicho cha bunge  na kutoka nje.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com