HALMASHAURI ZAKUSANYA BIL 449 MAPATO YA NDANI

Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI

IKIWA imepita robo tatu ya mwaka wa fedha 2018/2019, halmashauri zote zimekusanya Sh bilioni 449.8 ambayo ni asilimia 61 kati ya Sh bilioni 735.6 kutoka kwenye vyanzo vya ndani huku Halmashauri ya Jiji la Dodoma na Mkoa wa Dar es Salaam zikiongoza kwa mapato ghafi.

Hayo yabamebainishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa alipokuwa akitoa taarifa za makusanya kwa halmashauri kuanzia Juni mwaka jana hadi Machi mwaka huu na kusisitiza kuwa vyanzo vya mapato vinavyokuswanywa na serikali kuu havijumuishi katika makusanyo hayo.

Akifafanua zaidi Jafo alisema halmashauri tano zilizoongoza kwa kigezo cha asilimia ya mapato ya ndani kuwa ni Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi(asilimia 113), Geita (asilimia 109), Wanging’ombe(asilimia 105), Kilolo (asilimia 103) na Sumbawanga (asilimia 92) huku zile zilizofanya vibaya kuwa ni Newala na Tandahimba (asilimia 15), Momba na Masasi (asilimia 13) na Nanyamba (asilimia 12)

Kwa kigezo cha pato ghafi, Jafo alisema halmashauri zinazongoza kwa wingi wa mapato kuwa ni Halmashauri ya Jiji la Dodoma 9 (Sh bilioni 49.9), Ilala (Sh bilioni 44.8), Kinondoni(Sh bilioni 23.5) Temeke Sh bilioni 20.6) na Jiji la Arusha (Sh bilioni 12.5) wakati halmashauri tano zilizofanya vibaya katika kundi hili ni Madaba(Sh milioni 293.7), Newala (Sh milioni 268.3) Kakonko (Sh milioni 238.6) Buhigwe (Sh milioni 177.3) na Momba(Sh milioni 170.4).

Aidha, katika kundi la mikoa kwa kigezo cha asilimia, Jafo alisema mikoa inayoongoza kwa kigezo cha asilimia ya mapato ya ndani ni Mkoa wa Iringa (asilimia 77), Geita (asilimia 73), Dar es salaam (asilimia 72), Dodoma na Songwe (asilimia 68) wakati mikoa iliyofanya vibaya katika kundi hili ni Shinyanga (asilimia 46), Katavi (asilimia 43), Kigoma na Lindi (asilimia 42) na Mtwara (asilimia 26).

Kwa upande wa mikoa kwa kigezo cha pato ghafi, Jafo alitaja mikoa inayoongoza kuwa ni Dar es Salaam (Sh bilioni118.4) Dodoma (Sh bilioni 57.30), Mwanza (Sh bilioni 22.9) Arusha (Sh bilioni 22.8) na Mbeya (Sh bilioni 19.8) wakati mikoa iliyofanya vibaya katika kundi hili ni Manyara (Sh bilioni 6.5) Lindi (Sh bilioni 6.1), Rukwa (Sh bilioni 5.8) Kigoma (Sh bilioni 4.5) na Katavi Sh bilioni 3.8).

Aidha, Jafo alisema Jiji la Dar es Salaam linaongoza katika kundi la halmashauri za majiji kwa asilimia kwa kukusanya asilimia 87 ya makisio huku jiji la Tanga likiwa la mwisho katikakundi hilo baada ya kukusanya asilimia 57 ya makisio.

Alisema Halmashauri ya Dodoma inaongeza kwa kigezo cha patoghafi ambapo imekusanya Sh bilioni 50 na halmashauri ya jiji la Tanga imekuwa ya mwisho baada ya kukusanya Sh bilioni 8.7.

Aidha, Jafo alisema halmashauri ya manispaa ya Sumbawanga imeongoza kundi la halmashauri za Manispaa kwa kukusanya asilimia 92 ya makisio huku Lindi ikishika nafasi ya mwisho kwa kukusanya asilimi 23 ya makisio.

Jafo alisema kwa upande wa halmashauri ya Manispaa ya Ilala imeoongoza katika kundi la halmashauri za Manispaa kwa kigezo cha mapato ghafi baada ya kukusanyw Sh bilioni 50 huku Tanga ikiwa ya mwisho kwa kukusanya Sh bilioni 8.7.

Aidha, JAfo alisema halmashauri ya Mji wa Kondoa imeongoeza kundi la halmashauri za miji kwa kigezo cha asilimia ambapo wamekusanya kwa asilimia 92 ya makisio huku halmashauri ya Mji wa Nanyamba imekuwa ya mwisho baada ya kukusanya asilimi 12 ya makisio.

“ Katika kigezo ya pato ghafi kwa halmashauri za mji, Geita inaongeza baada ya kukusanya Sh bilioni 5.9 na halmashauri ya mji wa Nanyamba imekuwa ya mwisho ikiwa imekusanya Shilingi milioni 293.9.

Kwa upande wa halmashauri za wilaya, Jafo alisema Mbozi inaongoza kwa kukusanya kwa asilimia 113 ya kamkisio nay a mwisho ni Masasi iliyokusanya asilimia 13 ya makisio wakati kwa upadne wa pato ghafi, Chalinze inaoongoza kwa kukusanya Sh bilioni 4.6 na ya mwisho katika kundi hili ni Momba iliyokusanya Sh milioni 170.4.

Aidha, Jafo aliwataka wakurugenzi ambao makusanyao yao hayajafika asilimia 50 kuaza kujitathimini huku asikisisitiza kuwapo taarifa za baadhi ya watumishi kuhujumu ukusanyaji wa mapato.

“ Mkurugenzi usikubali kurudishwa nyuma na watendaji wasio waamini, maana kuna baadhi ya maeneo watu wamekuwa wahatumii mifumo ukusanyaji wa mapato kwa njia ya kieletroniki na wengine hawatumii kabisa,”

Aidha, Jafo ameendelea kusisitiza wakurugenzi kuhakikisha fedha za mapato ya ndani asilimia 40 au 60 kuelekezwe kwenye miradi ya maendeleo eneo husika sambamba na utoaji wa asilimia 10 za fedha za ndani kwa walemavu, vijana na wanawake na kusisitiza kuwa mwisho wa mwaka mambo hayao yatakuwa ni tathimini ya utendaji wa wakurugenzi hao.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
أحدث أقدم