Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

JESHI LA ZIMAMOTO TANZANIA LATOA TAHADHARI SIKUKUU YA PASAKA


Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania limesema limejipanga vyema kupambana na majanga katika kipindi hiki cha Sikukuu ya Pasaka huku likitoa wito kwa Watanzania kuchukua tahadhari katika matumizi ya vifaa vya kielektroniki.

Taarifa iliyotolewa leo Ijumaa Aprili 19, 2019 inaeleza kuwa jeshi hilo litakuwa imara kushirikiana na watoa huduma wengine katika mikoa yote ya nchi.

“Tunapoelekea kipindi hiki cha Sikukuu ya Pasaka, Jeshi la Zimamoto na uokoaji katika mikoa yote linawahakikishia wananchi limejipanga kikamilifu kuhakikisha sikukuu hii inasherehekewa bila kuwa na majanga ya moto yanayoweza kuathiri maisha na mali za Watanzania,” inaeleza taarifa hiyo.

Taarifa hiyo inasema jeshi lipo imara na litaendelea kuelimisha umma kuzingatia kinga na tahadhari dhidi ya moto ili kuhakikisha maisha na mali za Watanzania zinakuwa salama.

“Tunatoa rai kwa Watanzania kuchukua tahadhari hasa katika matumizi ya vifaa vya kielektroniki kwa sasa vinatumika mpaka ngazi ya familia. Janga la moto huzuka endapo kitapatikana chakula cha moto, joto la kutosha na hewa ya oksijeni,” inasema taarifa hiyo.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com