WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amesema hajawahi kumuona mtu muongo katika nchi hii kama Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad.
Amesema kwamba taarifa iliyotolewa na CAG katika ukaguzi wake kwamba Jeshi la Polisi liliagiza sare hewa za polisi haina ukweli wowote kwa kuwa sare hizo zipo na ziko kwenye makontena katika ghala kuu la polisi.
Ili kuthibitisha kauli yake,Waziri Kangi alisema yuko tayari kwenda kutembelea ghala hilo na kama sare hizo hazitakuwemo, uwaziri wake ana uweka rehani.
“Sijawahi kuona mtu muongo kama CAG, Jeshi la Polisi hakuna sare hewa. Ninaomba maofisa wa ofisi ya CAG twende nao stoo wakaone sare mpya za jeshi la polisi. Kama nasema uongo nitajivua nguo na ninaweka uwaziri wangu rehani” Alisema Kangi Lugola jana bungeni alipokuwa akihitimisha mjadala wa hotuba ya bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2019/20.
Pamoja na hayo,Waziri Kangi aliwataka wabunge wamuogope Mungu na kwamba wasipende kushabikia mambo yasiyokuwa na ukweli wowote na kwamba watu wasiokuwa wakweli waogopwe kama ukoma
Social Plugin