Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imemtaka Katibu Mkuu CHADEMA , Dk Vicent Mashinji kuieleza mahakama kwa nini ameshindwa kuhudhuria kesi yake iliyopo mahakamani hapo.
Dk Mashinji ambaye ni mshtakiwa wa sita katika kesi ya kufanya mikusanyiko isiyo halali, inayowakabili vigogo tisa wa chama hicho, ameshindwa kufika mahakamani hapo kwa kile kilichoelezwa yupo kwenye kesi nyingine iliyopo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Songea mkoani Ruvuma.
Dk Mashinji ametakiwa kufika mahakamani hapo Aprili 17, 2019 na kuieleza mahakama hiyo sababu za yeye kushindwa kufika mahakamani hapo, wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kuanza kusikiliza ushahidi wa upande wa mashtaka.
Dk Mashinji na wenzake wanakabiliwa na makosa 13 likiwemo la kula njama, ambapo wote wanadaiwa kuwa, Februari 1 na 16, 2018, Dar es Salaam walikuĺa njama ya kutenda kosa la kufanya mkusanyiko usio halali na kukiuka tamko la kutawanyika.
Social Plugin