MWANAMKE ALIYEKANA KUWA 'SIYO MJAMZITO' AJIFUNGUA CHOONI


Mwanamke wa miaka 23 amejifungua mtoto akiwa kwenye choo licha ya kukana mara kadhaa kwamba hakuwa mjamzito. 


Emmanuella Osei ambaye anaishi Pennsylvania, Marekani alijifungua akiwa kazini Jumamosi Machi 30,2019.

 Kulingana na jarida la Daily Mail, mtoto huyo alinusurika kifo baada ya maafisa wa polisi kufika eneo la tukio na kumuokoa.

 Emmanuella tayari yuko na mtoto mwingine wa miaka miwili nyumbani kwao nchini Ghana na hakuwahi kuwwambia jamaa yake kwamba alikuwa mjamzito.

 Alipozidiwa na uchungu wa kujifungua, Emmanuela alimwambia meneja wake apige nambari ya dharura 911 ila hakumwelezea kwamba alikuwa amejifungua. 

Polisi waliikuta damu ikiwa imejaa kwenye sakafu huku akiwa na muimivu mengi na mwanawe pia akiwa ameachwa sakafuni bila hata kufunikwa chochote. 

Inaelezwa kuwa Emmanuela alitaka mtoto huyo afe kwani alikuwa amemuacha ndani ya maji kwa zaidi ya dakika 10. 

Mtoto huyo alikimbizwa hospitalini akiwa hali mahututi ila alipata nafuu baada ya kutibiwa.

 Emmanuela alikamatwa na maafisa wa polisi na iwapo atapatikana na hatia, atahukumiwa kifungo cha miaka 10. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم