Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

JAMAA ALIYEMPA UJAUZITO MWANAE AFUMANIWA 'LIVE' AKIFANYA NGONO NA MBUZI WA JIRANI YAKE


Jamaa mmoja (45) huko Kakamega nchini Kenya  anauguza majeraha mabaya baada ya kupokezwa kichapo cha mbwa koko na wenyeji waliojawa na hamaki baada ya kufumania peupe akishiriki ngono na mbuzi wa jirani.


Jamaa huyo alikiona na mtema kuni baada ya kufumaniwa akichovya asali katika mzinga usiostahili huku ikidaiwa kuwa hii sio mara ya kwanza na kwamba mwanaume huyo amekuwa akishiriki mapenzi na wanyama kwa muda mrefu. 

 Kwa mujibu wa mdokezi aliyezungumza na mwandishi wa habari hizi ni kwamba, jamaa huyo maarufu Jokinda kutoka kijiji cha Rostaman eneo bunge la Lurambi Kaunti ya Kakamega alikutwa akifanya kitendo hicho usiku wa Jumatano, Aprili 10,2019 baada ya jirani kumsikia mbuzi wake akitoa sauti zisizokuwa za kawaida.

 Alipokwenda kuangalia kilichokuwa kikiendelea, alipigwa na butwaa kubwa alipomuona mwanaume huyo akiwa juu ya mbuzi wake.

Mke wa mshukiwa (jina linahifadhiwa) alisema kuwa, maisha yao ya ndoa yamekuwa na taabu nyingi na mume wake amekuwa akimtimua kila mara.

 Kulingana naye, mume wake amekuwa akimtunza mbuzi huyo kama kitu cha thamani sana na tabia hiyo imekuwa ikimshangaza hadi mumewe alipofumaniwa akifanya kitendo hicho.

 "Kwa muda mrefu tumekuwa tukijiuliza mbona mume wangu amekuwa akimpenda sana mbuzi huyu. Mara nyingine utamuona anampeleka malishoni bila kuambiwa na mtu yeyote ikizingatiwa kuwa mbuzi huyo si wetu...

"Na ikifika jioni anapenda kumfunga karibu na boma letu, leo ndio tumejua ukweli wa mambo amepatikana juu ya mbuzi na tunaushuku ujauzito ambao mbuzi huyo ako nao ni wake," alisema mwanamke huyo. 

Zaidi ya kufanya mapenzi na mbuzi wa jirani, inadaiwa Jokinda amekuwa akimbaka mwanawe mwenye umri wa miaka 15 ambaye akili zake si timamu na hata amepachika mimba. 

"Huyu mzee ana tabia mbaya kila mara akinifukuza amekuwa na mazoea ya kulala na mwanangu na hata akampachika mimba. Nashangaa ni nini simpi ndio lazima afanye hivyo" aliongezea. 

 Hata hivyo wazee katika eneo hilo wamewataka maafisa wa polisi kumchukulia mshukiwa huyo hatua kali za kisheria ili iwe funzo kwa wengine wanaofanya vitendo vya aina hiyo. 

"Hii ni laana kwa jamii tunatakiwa kufanya tambiko ili kufukuza mazimwi haya. Mshukiwa anapaswa kuchukulia hatua kali za kisheria ili wengine wenye tabia kama zake kukoma, hata hafai kuruhusiwa kurudi katika familia yake." alisema mmoja wa jamaa kwa jina Chrispinus. 

Ripoti ya Dennis Avokoywa – Kakamega 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com