Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu imemhukumu Mwita Daudi kwenda jela miaka 3 kwa kosa la kumtorosha binti kutoka kwa wazazi wake kwa nia ya kumuoa.
Akizungumza Mahakamani Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Nassib Swedi amesema mtuhumiwa alitenda kosa hilo Februari 03 mwaka huu, saa 11 jioni huko katika Kijiji cha Mandela wilayani Maswa.
Ameongeza kuwa kuwa Mwita Daudi alitenda kosa la kumtorosha binti huyo kutoka kwa wazazi wake kwa nia ya kutaka kumuoa.
Akijitetea kabla ya kuhukumiwa na Mahakama alikiri kutenda kosa hilo na kuiomba mahakama impunguzie adhabu kuwa ni kosa lake la kwanza na hakukusudia kufanya hivyo na anategemewa na familia.
Social Plugin