Ikulu ya Marekani imetangaza kuyawekea vikwazo mataifa yanayoendelea kununua mafuta kutoka Iran katika juhudi za kuongeza mbinyo kwa taifa hilo la Kiislamu linalouza mafuta kwa wingi duniani.
Kwenye taarifa iliyotolewa na ikulu ya White House Rais Donald Trump amesema ameamua kutoongeza muda wa kuzisamehe vikwazo hivyo baadhi ya nchi washirika baada ya kufikia muda wake wa mwisho mapema mwezi ujao.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa hatua hiyo inalenga kuifanya Iran isiuze kabisa mafuta nje ili kuikosesha nchi hiyo mapato yatokanayo na bidhaa hiyo ambayo ndio chanzo chake kikuu cha fedha za kigeni.
Saudi Arabia kwa upande wake imesema iko tayari kuweka uthabiti katika soko la mafuta baada ya hatua hiyo ya Marekani hii ikiwa ni kulingana na waziri wa mafuta wa nchi hiyo Khalid al-Falih.
Social Plugin