Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

HAWA NDIYO WANAWAKE 7 MATAJIRI ZAIDI DUNIANI...HII HAPA SIRI YA UTAJIRI WAO

MacKenzie Bezos will keep a 4% stake in Amazon

Wakati mwanaume tajiri zaidi duniani anapoamua kuachana na mke hana budi kugawana sehemu ya mali yake na mtalaka wake.

Hilo limedhihirika wiki hii baada ya mwanzilishi wa shirika la Amazon Jeff Bezos, kukubaliana kuhusu masharti ya MacKenzie kutengana kwao.

MacKenzie Bezos atasalia na 4% ya mapato ya shirika hilo kubwa zaidi linaloendesha biashara yake mtandaoni.

Thamani ya utajiri wa Bi MacKenzie unakadiriwa kuwa dola bilioni $35.6 (£27bn), hali ambayo imemfanya kuwa mwana mke wa tatu tajiri duniani (na mtu wa 24 tajiri zaidi duniani).

Je wanawake wengine katika orodha hiyo ni kina nani na walifika vipi hapo?

1) Françoise Bettencourt-Meyers
Thamani yake : Dola bilioni 49.3, ni mtu wa 15 tajiri zaidi duniani kwa mujibu wa jarida la Fobes.

Yeye ni nani?

Ni mfaransa mrithi wa kampuni ya vipodozi ya L'Oréal ambaye anamiliki 33% ya kampuni hiyo na familia yake.

Mwanamke huyo wa miaka 65 alirithi mali utajiri huo kutoka kwa mama yake Liliane Bettencourt, aliefariki dunia mwezi Septemba mwaka 2017 akiwa na miaka 94.

Wawili hao walizozana kwa miaka kumi kuhusiana na usimamizi wa kampuni hiyo hadi wakafikishana mahakamani mwaka 2007.

Bi Bettencourt-Meyers aliwasilisha kesi mahakamani akihoji kuwa washirika wa karbi na mama yake walikuwa wakimlaghai licha ya hali yake mbaya ya kiafya.

Lakini waliafikiana miaka kadhaa kabla ya kifo cha mama yake.

2) Alice Walton
Thamani yake : Dola biloni 44.4, thamani ambayo inamuorodhesha katika nafasi ya 17 ya watu tajiri zaidi duniani.

Yeye ni nani?

Mwanamke huyo aliye na umri wa miaka 69 ni binti wa kipekee wa mwanzilishi wa duka kubwa zaidi la jumla nchini Marekani,Sam Walton.

Hata hivyo tofauti na ndugu zake wawili wa kiume, alijitenga na biashara ya familia na kujiingiza katika biashara ya sanaa na kuwa mwenyekiti wa makavazi ya sanaa nchini Marekani inayofahamika kama Crystal Bridges Museum iliyo na makao yake mjini Bentonville, Arkansas.

3) MacKenzie Bezos
Thamani yake: Ni karibudola bilioni 35.6 -ndio thamani yake katika kampuni ya Amazon pekeea, lakini thamani yake halisi inatarajiwa kuwa juu zaidi.

Fuatilia kwa karibu orodha ya jarida la Forbes la watu tajiri zaidi duniani mwaka 2020 kujua thamani yake halisi ni gani.

Yeye ni nani?

Mama huyo wa miaka 48 amezaa watoto wanne na mwasisi wa shirika la Amazon, ambaye alimuoa mwaka 1993 walipokua wakifanya kazi pamoja katika hazina ya hedge.

Mkaazi huyo wa California alikua miongoni mwa wafanyikazi wa kwanza wa kampuni ya Amazon, na alijiunga nalo kama mhasibu.

4) Jacqueline Mars
Thamani yake: Ni dolaola bilioni 23.9 - ni mtu wa 33 tajiri zaidi duniani kabla ya enzi ya MacKenzie Bezos ( sawa na wanawake wengine katika orodha inayofuata hapo chini).

Yeye ni nani?

Mwanamama huyu wa miaka 79 ni mzaliwa wa tatu katika familia ya Mars, kampuni kubwa zaidi ya uokaji dunia ambayo alianzishwa na babu yake Frank mwaka 1911.

Alifanya kazi katika kampuni ya familia yake kwa karibu miaka 20 nakuwa katika bodi ya usimamizi wake hadi mwaka 2016.

5) Yan Huiyan

Thamani yake: Dola bilioni22.1, thanai ambayo inamfanya kuwa mwanamke tajiri zaidi nchini China na mtu wa 42 tajiri zaidi duniani.

Yeye ni nani?

Mwanadada huyu mwenye umri wa miaka 37 anamiliki hisa katika kampuni kubwa ya ujenzi nchini China inayofahamika kama Coutry Garden Holdings, ambayo inaongoza katika biashara ya sekta ya ujenzi China.

Kwa mujibu wa utafiti Country Garden, ilikua kampuni kubwa zaidi ya ujenzi kote duniani mwaka 2016.

Yan Huiyan, amerithi 57% ya hisa ya kampuni hiyo kutoka kwa baba yake.

6) Susanne Klatten
Thamani yake : Ni dola bilioni 21, ambayo inamweka katika nafasi ya 46 ya watu tajiri zaidi duniani.

Yeye ni nani?

Ni mtu wa pili kutoka barani Ulaya katika orodha ya watu tajiri zaidi duniani.

Mwanamke huyu raia wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 56 ana mchanagnyiko wa magari na makampuni ya dawa.

Alirithi 50% ya kampuni ya kutengeneza dawa ya Altana AG wakati wazazi wake walipofariki, huku ndugu yake wa kiume akimiliki 50% ya kampuni ya uundaji magari ya BMW.

Hata hivyo ameifanya kampuni ya Altana kuwa yake binafsi baada ya kununua hisa zote za kampuni zingine kubwa.

7) Laurene Powell Jobs
Thamani yake: Ni dola bilioni 18.6, thamani inayomfanya kuwa mtu wa 54 tajiri zaidi duniani.

Yeye ni nani?

Ni mjane wa mwanzilishi wa kampuni kubwa ya teknolojia ya Marekani Apple, Steve Jobs.

Familia yake ilimiliki takriban dola bilioni 20bn katika kampuni za Apple na Disney wakati mume wake alipofariki dunia.

Tangu wakati huo, Bi.Laurene mwenye umri wa miaka 55 aliendelea mbele na kukuza utajiri wake kwa kuwekeza sehemu ya fedha zake katika sekta ya habari, kwa kumili hisa nyingi katika jarida la Atlantic , pamoja na uchapishaji wa wa majarida ya Mother Jones na ProPublica.
Chanzo - BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com