MREMBO AUAWA KWA KUPASULIWA KICHWA KWA SHOKA NA MPENZI WAKE... MUUAJI ASEMA BINTI KALA SANA PESA ZAKE

Hali ya taharuki imetanda katika hospitali ya rufaa na mafunzo ya Moi mjini Eldoret nchini Kenya baada ya jamaa mmoja aliyejulikana kwa jina la Naftali Njahi Kinuthia (28) aliyejihami kwa shoka na kisu kumvamia na kumkata kwa shoka kichwani mwanafunzi wa taaluma ya uuguzi Ivy Wangechi (28) anayesomea katika Chuo Kikuu cha Moi.

 Inaripotiwa kuwa, mwanamme huyo anayedaiwa kuwa mpenzi wake alikuwa amebeba shoka alilokuwa amelitia makali pamoja na kisu katika gunia, wakati alikuwa akimsubiri mwanadada huyo katika lango la hospitali hiyo Jumanne Aprili 9, 2019.

 Jamaa huyo alikamatwa na wahudumu wa boda boda na baadhi ya wanafunzi ambao walimpa kichapo cha mbwa koko na kumwacha na majeraha mabaya, kabla yake kuokolewa na maafisa wa polisi na kumpeleka katika hosptali ya rufaa ya Moi, Eldoret kwa ajili ya matibabu.
 Walioshuhudia tukio hilo walisema kuwa, mshukiwa alimgonga kwa shoka kichwani marehemu kabla ya kumgeukia na kumchinja. 

Mwanadada huyo ambaye ni mwanafunzi wa chuo cha Moi kilichoko mkabala na hospitali hiyo, na alikuwa katika mwaka wake wa sita katika taaluma ya uuguzi na tukio hilo lilitokea wakati mwanafunzi huyo alikuwa ametoka hospitalini humo kuwahudumia wagonjwa katika wadi.


Uchunguzi wa maiti umeonyesha kuwa mwanafunzi wa chuo kikuu cha Moi aliyeuawa kinyama na mpenziwe alivuja damu nyingi.

Benson Macharia, mwanapatholojia aliyefanya uchunguzi huo alisema marehemu alikuwa na majeraha mabaya kwenye shingo na kichwani.

"Uchunguzi wa maiti umeonyesha kuwa Ivy alipata majeraha mabaya kwenye upande wake wa kushoto wa shingo ambayo yalikata mishipa ya kusukuma damu kwenye ubongo, na pia sehemu ya mifupa kwenye shingo lake kuvunjika,"Macharia alisema.


Naftali Njahi Kinuthia, jamaa anaye kisiwa kumuua kinyama mwanafunzi wa chuo kikuu cha Moi hatimaye amezungumza na kufichua sababu zilizomfanya atekeleze uhayawani huo.

 Kulingana na Njahi mwenye umri wa miaka 28, msukumo wa kutenda uhayawani huo ulitokana na hatua ya binti huyo kumpuuza mara kwa mara. 

Kulingana na taarifa ya Citizen, mnamo Jumatano, Aprili 10, Njahi aliwaambia maafisa wa upelelezi kuwa alikuwa ametumia fedha zake na vile vile kuwekeza hisia zake ili penzi lao linawiri, lakini alisikitishwa kuwa binti huyo alimpuuza.

 Matamshi ya jamaa huyo yalithibitishwa na mkuu wa DCI eneo la Eldoret Mashariki, Ali Kingi, aliyefichua kuwa mshukiwa angali anapokea matibabu katika hospitali ya mafunzo na rufaa ya Moi.

Mshukiwa alihoji kuwa, awali alikuwa amemtumia Ivy pesa ambazo alimwitisha akilenga kuandaa sherehe ya siku ya kuzaliwa kwake, lakini baada ya binti huyo kupokea fedha hizo alikaa kimya, hivyo basi akalazimika kusafiri kutoka Thika hadi Eldoret ili kutafuta majibu.

 "Mshukiwa alisema kwamba alimtumia binti huyo pesa kwa mara nyingi mno. Mwanadada huyo awali alikuwa amemtumia mshukiwa pesa za kuandaa sherehe ya siku ya kuzaliwa kwake. 

Baada ya jamaa kutuma pesa, Ivy alianza kudinda kupokea simu zake. Ilimbidi Kinuthia kufunga safari kutoka mjini Thika hadi Eldoret akinuia kutafuta jawabu kutokana na hatua ya Ivy ya kumpuuza," alisema Kingi. 

 Taarifa ya Citizen ilisema kuwa, mnamo Jumatano, Aprili 10, Njahi aliwaambia maafisa wa polisi alikuwa ametumia fedha zake halikadhalika kuwekeza hisia zake ili penzi lao linawiri, lakini alisikitishwa kuwa marehemu alimpuuza.

 "Alifichua kuwa hii sio mara yake ya kwanza kuzuru mji wa Eldoret akitaka kumwona mpenziwake. 

Mara ya mwisho wakiwa pamoja siku ya Ijumaa, binti huyo aliharakisha mkutano wao ambao ulichukua muda mfupi, akidai kuwa alikuwa anaelekea katika makazi yao ya wanafunzi kuvua sare yake ya kazi.

Baadaye Ivy alizima simu yake asipatikane tena," Kingi alisema. 

DCI aidha ilithibitisha kuwa, wazazi wake Ivy walimfahamu jamaa huyo kwani alikuwa rafiki wa kifamilia kwa muda mrefu.

 Njahi angalia anapokea matibabu katika hospitali ya rufaa ya Moi, chini ya ulinzi mkali baada ya umati ulikouwa na hamaki kumshambulia baada ya kutekeleza mauaji hayo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post