Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde ameshauri Serikali isifanye uchaguzi wa kipengele cha Urais katika uchaguzi mkuu wa 2010 na badala yake iruhusu uchaguzi uhusishe Wabunge na Madiwani pekee.
Akizungumza jana Bungeni amesema ni kutokana na kwamba Rais John Magufuli hana mpinzani kwa sasa na badala yake fedha ambazo zinatarajiwa kutumika katika uchaguzi huo zitumike katika kujenga nchi.
“Kuna faida gani kwenda kupoteza fedha chungu mzima kwa ajili ya uchaguzi Rais ambaye hana mpinzani, tufanye uchaguzi wa Udiwani na Ubunge kwenye Urais tuache na hizo pesa za uchaguzi tumkabidhi Rais zisaidie kuboresha kujenga Nchi,” amesema Lusinde.