Mbunge wa Malindi (CUF), Ali Saleh amezungumzia kitendo cha wapinzani kuporwa wabunge kwamba kinadidimiza demokrasia nchini.
Akichangia hotuba ya makadirio ofisi ya Waziri Mkuu leo Jumatatu Aprili 8, 2019 Saleh amesema hakuna uhuru kwa vyama vya siasa nchini.
Saleh amesema inasikitisha kuona viongozi wa CCM wanaendelea kufanya mikutano huku wapinzani wakielezwa kuhusu masuala ya kiintelejensia,
Huku akikatizwa na taarifa kutoka kwa wabunge wenzake, Saleh amesema CCM kinatawala lakini hakiongozi kutokana na yale yanayofanyika nchini.
Mbunge huyo ameitaka Serikali na viongozi kubadilika na kutoa haki kwa kila upande.
Social Plugin