Mbunge wa Ulanga(CCM), Goodluck Mlinga ametaka wakuu wa mikoa na wilaya waliofanya vizuri katika utendaji wao kupewa tuzo za utendaji bora.
Mlinga amewataja baadhi ya wakuu mikoa kuwa ni Ally Hapi (Iringa), Mrisho Gambo (Arusha), Paul Makonda (Dar es Salaam) na Alexender Mnyeti (Manyara).
Hivyo, akahoji Wizara ina mpango gani wa kuwaandalia motisha au Tuzo Wakuu hao wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya ambao wanafanya kazi vizuri.
Swali hilo limejibiwa na Waziri wa Tamisemi, Selemani Jafo ambapo amesema kuwa tayari suala hilo lipo katika ajenda za vikao vinavyoendelea kwani ni kweli anatambua juhudi zinazofanywa na baadhi ya wakuu wa mikoa na wakuu wilaya kwani kwa kiasi kikubwa matatizo mengi ya wananchi yamepungua.
”Nikiri wazi kweli kuna wakuu wa mikoa hivi sasa wanaofanya kazi vizuri sana, ajenda ya kuwapa motisha kwa baadhi ya wakuu wa mikoa tumeshaanza kuifanya katika vikao vyetu, na juzi baadhi ya Wakuu wa Mikoa tumewapa vyeti kwa jinsi gani wanasimamia mambo ya serikali vizuri” amesema Jafo
Social Plugin