Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MKE WA MHUBIRI AFARIKI DUNIA KWA KUUMWA NYOKA BAADA YA HARUSI

Mhubiri mmoja kutoka Nigeria anaomboleza kifo cha mkewe kilichotokea siku moja tu baada ya wawili hao kufanya harusi.


 Mwanzilishi wa kanisa la Miracle Working God Ministry, Patrick Ayaefe alisema mkewe alifariki baada ya kuumwa na nyoka. 

Kulingana na taarifa za jarida la Ghanaweb.com, wanandoa hao walikuwa wamekaa katika ndoa kwa miaka minane kabla ya kuamua kuhalalisha ndoa yao Aprili 2,2019.

Mhubiri huyo mwenye umri wa miaka 44 aliambia jarida hilo kwamba mkewe amemuacha na watoto wanne na hajui atakapoanzia kuwalea.

"Tulikuwa tumempumzika tu nyumbani kwetu mwendo wa saa moja jioni baada ya harusi yetu, mke wangu aliondoka na baada ya dakika tano nilisikia akipiga nduru, nilipofika mahali alipokuwa nilipata kama ameumwa na nyoka," Mhubiri huyo alisema.
Mhubiri huyo alimkimbiza mkewe hospitalini lakini aliaga dunia kabla ya kuhudumiwa na madaktari.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com