LEMA ACHAFUA HEWA..WABUNGE WA UPINZANI WATOKA NJE YA BUNGE

Baadhi ya wabunge wa vyama vya upinzani bungeni jijini Dodoma, wamekasirishwa na hatua ya Dk. Tulia Ackson, Naibu Spika kuagiza kwamba, Godbless Lema, Mbunge wa Arusha Mjini kuhojiwa na Kamati ya Maadili na Madaraka ya Bunge kwa kuunga mkono kuwa Bunge ni dhaifu.

Dh. Tulia amechukua uamuzi huo leo tarehe 2 Aprili 2019 baada ya Lema kusema bunge ni dhaifu, wakati akichangia mjadala kuhusu ripoti ya mahojiano ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad na Kamati ya Maadili na Madaraka ya Bunge. 

“Kwa mameno hayo uliyosema, na wewe unapelekwa kwenye kamati ya madili, na ukae hamna mchango tena. Sababu tunajadili adhabu kuhusu maneno hayo (ya CAG) nawe unasema, unathibitisha.

“… na wewe utaelekea kwenye kamati hiyo ukathibitishe vizuri kule, kwa hiyo kamati na huyu naye analetwa kwenu kwa utaratibu wa kawaida,” amesema Dk. Tulia.

Hata hivyo, wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na wachache wa Chama cha Wananchi (CUF) waliamua kutoka nje kuonesha namna walivyokasirishwa na hatua ya Dk. Tulia.

Akichangia mjadala huo, Lema alisema kuwa Hamila Mdee, Mbunge wa Kawe jijini Dar es Salaam hakutendewa haki kutokana na bunge hilo kutaka (Mdee) asimamishwe kuhudhuria vikao viwili kutokana na kuunga mkono kauli ya CAG.

Chanzo- Mwanahalisi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم