Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Jana April 16, 2019 ajali kubwa ya Moto ilitokea katika jengo la mfanyabiashara Jijini Dodoma , Franscis Maiko Shio lililo mkabala na Bahi Hotel jirani na Nyerere Square hali iliyolazimu jeshi la zimamoto mkoa wa Dodoma kufika katika eneo la tukio na kufanikiwa kuokoa mali mbalimbali.
Kamanda wa jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Dodoma A.C.F Fikiri Salehe Salla amesema walizipokea taarifa za ajali hiyo ya moto jana majira saa 2:16 asubuhi na wakatuma gari la kwanza saa 2:19 asubuhi.
Amefafanua kuwa baada ya kuona tukio la ajali ya moto ni kubwa waliongeza magari matatu ya zimamoto na askari 14 na maafisa watano ambao walifanikiwa kuuzima moto huo baada ya robo saa.
Aidha ,amesema chanzo cha ajali ya moto huo ni hitilafu ya umeme huku uchunguzi ukiwa unaendelea zaidi.
Kamanda Salla ametoa wito kwa wananchi kuitumia namba ya bure 114 pindi wanapopatwa na mikasa ya ajali ya moto huku akitahadharisha kila nyumba kuwa na vifaa vidogovidogo vya kuzimia moto pamoja na kujenga nyumba zenye mpangilio maalum ili kuruhusu miundombinu kufikika haraka jeshi hilo pindi panapotokea ajali.
Vilevile Kamanda Salla amelishukuru Jeshi la polisi mkoa wa Dodoma kwa kuweza kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kuhakikisha mali zilizokuwa zinaokolewa haziibiwi.
Mali zilizookolewa kutokana na ajali ya moto huo ni TV Screen kadhaa,Nguo,Kabati,viatu na vingine vingi huku hakuna majeruhi au vifo vyovyote vilivyoripotiwa kutokana na ajali hiyo na uchunguzi unaendelea juu ya samani au fedha zilizoharibika au kupotea kutokana na ajali hiyo ya moto.
Social Plugin