MVUA YA KENYA 'IMEKWAMA NCHINI TANZANIA' ... TAHADHARI YA MAFURIKO YATOLEWA

Idara ya hali ya nga nchini Kenya imesema kuwa upepo unaofaa kushinikiza mvua kunyesha nchini umekwama nchini Tanzania. 

Kaimu mkurugenzi wa idara hiyo Stella Aura amesema kuwa mvua hiyo 'imekwama' nchini Tanzania kwa kukosa shinikizo la kuisukuma upande wa juu .

 Amesema hali hii itashuhudiwa hadi mwishoni mwa Aprili,2019 huku akionya kuwa huenda kukawa na mafuriko katika nyanda za nchini wakati mvua itakapoanza kunyesha 

Idara hiyo imewahimiza wakulima kupanda mimea ambayo inaweza stahimili makali ya kiangazi. 

Idara hiyo ilifichua kuwa huenda hali hii ya kiangazi ikasalia hivyo hadi mwishoni mwa mwezi wa Aprili 2019, ambapo mvua kubwa inatarajiwa kuanza japo kwa muda mfupi.

Kulingana na kaimu mkurugenzi wa idara hio Stella Aura, itachukua muda kabla upepo huo kupata nguvu za kuisUkuma mvua kuelekea nyanda za Kaskazini. 

"Mvua imesalia nchini Tanzania, kutokana na kukosa shinikizo la kutosha la kuyasukumu mawimbi ya kuleta mvua nchini Kenya. Mvua itachelewa kunyesha kwa muda lakini hali hiyo itabadilika ifikiapo mwishoni mwa mwezi wa Aprili," Aura alifichua. 

Hata hivyo, alifichua kuwa mvua kubwa itashuhudiwa na huenda kukawa na mafuriko, hivyo basi aliwaonya watu wanaoishi katika nyanda za chini na vile vile wale wanaoishi katika mikondo ya maji kutafuta suluhu ya mapema kabla ya msimu huo.

Sehemu za Magharibi mwa Kenya zitashuhudia vipindi vya jua vikiambatana na ngurumo za radi, huku baadhi ya sehemu za Murang'a na Meru zikishuhudia maporomoko ya ardhi. 

Wakati huo huo tahadhari pia imetolewa kwa wakaazi wa maeneo ya Bundalang'i ambayo hushuhudia mafuriko kila kukinyesha. 

"Mvua kubwa haitanyesha jinsi tulishuhudia mwaka jana. Mara kwa mara mvua ikichelewa kunyesha huwa kunatokea mafuriko japo sio mazito ambayo pia hayachukui muda. Hata hivyo, ni vyema tahadahari ya mapema ichukuliwe ili kusishududiwe maafa na watu kupoteza mali yao," Idara hiyo ilisema.

 Idara hiyo iliwahimiza wakulima kupanda mimea iliyo na uwezo wa kustahimili kiangazi kwa kuwa mvua imekuwa sio ya kutegemewa tena. 

Wakulima aidha, wamesimulia hofu yao kutokana na hali ya anga na mvua kuchelewa kwani kwa kawaida, vipindi vya mvua hushuhudiwa kati ya miezi ya Machi, Aprili na May.

 Waziri wa Ugatuzi Eugene Wamalwa mnamo Jumatano, Aprili 10, alionya kuwa huenda kukawa na kiangazi mwaka huu kwani mvua imekuwa sio ya kutegemewa tena. 

Chanzo - Tuko

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post