MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, (PSSSF), umeendesha semina fupi kwa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kuhusu shughuli za Mfuko ikiwa ni miezi nane tangu kuanzishwa kwake.
PSSSF imeundwa kwa Sheria ya Utumishi wa Umma namba 2 iliyopitishwa na Bunge Januari 31, 2018 ambayo inaunganisha Mifuko minne ya Hifadhi ya Jamii ya GEPF, LAPF, PPF na PSPF.
Katika semina hiyo iliyofanyika Aprili 12, 2019, wajumbe walielimishwa kuhusu majukumu ya Mfuko, Wanachama wa Mfuko na Mafao yatolewayo na Mfuko.
Pichani ni Afisa Mkuu wa Matekelezo wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, (PSSSF), Bw. Mordgard Maten, (kulia), akitoa elimu kuhusu shughuli za Mfuko huo kwa wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), kwenye ukubi wa Karimjee jijini Dar es Salaam Aprili 12, 2019. Wakwanza kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Mamlaka hiyo, Mhandisi Japhet Maselle.
Afisa Mkuu wa Matekelezo wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, (PSSSF), Bw. Mordgard Maten (kulia), akizungumza wakati akiwasilisha mada kuhusu shughuli za Mfuko kwa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kwenye ukumbi nwa Karimjee jijini Dar es Salaam Aprili 12, 2019.
Afisa Mtekelezo Mwandamizi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, (PSSSF), Bw.Msafiri S. Mugaka (kulia), akiwa na Afisa Mkuu wa Matekelezo wa Mfuko huo, Bw. Mordgard Maten kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam Aprili 12, 2019.
Baadhi ya wajumbe wakisikiliza mada zilizokuwa zikitolewa na Maafisa wa PSSSF.
Mtendaji Mkuu wa TEMESA, Mhandisi Japhet Maselle (kulia), akiwa na baadhi ya viongozi wa baraza hilo wakisikilzia mada zilizokuwa zikitolewa na maafisa wa PSSSF.
Baadhi ya wajumbe wakisikiliza mada zilizokuwa zikitolewa na Maafisa wa PSSSF.
Afisa Uhsiano Mwandamizi wa PSSSF, Bw. Abdul Njaidi, akizunumza wakati wa semina hiyo.
Baadhi ya wajumbe wakisikiliza mada zilizokuwa zikitolewa na Maafisa wa PSSSF.
Maafisa wa PSSSF kutoka kushoto, Bw.Msafiri S. Mugaka, Bw. Abdul Njaidi na Bw.Donald Peter.
Mtendaji Mkuu wa TEMESA, Mhandisi Japhet Maselle (kulia), akizungumza wakati wa semina hiyo.
Mtendaji Mkuu wa TEMESA, Mhandisi Japhet Maselle (watatu kulia), na baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA, na maafisa waandiamizi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), mara baada ya kuwasilisha mada kuhusu shughuli za Mfuko kwa wajumbe wa Baraza hilo.
Social Plugin