Na. Amiri kilagalila, Njombe
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amekabidhi fedha kiasi cha shilingi milioni 10 kwa ajili ya kusaidia kukamilisha ujenzi wa Wodi ya kina mama katika kituo cha afya kifanya kilichopo halmashauri ya mji wa Njombe mkoani Njombe.
Rais Magufuli ametoa fedha hiyo mara baada ya kusikia changamoto ya afya inayowakabili wakazi wa kata hiyo, wakati akipokewa huku akitokea mkoani Ruvuma
"Hapa sasa hivi mmenieleza mmejenga kituo chenu cha afya na mmejenga wodi ya akina mama mmeshaezeka ila haijakamilika,mmenifurahisha kwa kuwa mmeanza vizuri hiyo wodi na mimi nawachangia milioni kumi ila zitumike vizuri,nitatuma watu wa kuja kuchunguza hizo milioni kumi zilivyoenda na atakayezila" alisema Magufuli
Aidha Rais Magufuli amesema anahitaji wodi hiyo ikajengwe kwa milioni kumi inatosha jengo hilo la akina mama huku akiagiza Tamisemi namna ya kuwapeleka manesi na madaktari mapema litakapokamilika jengo hilo.
Naye Mbunge wa jimbo la Njombe Mjini, Edward France Mwalongo ameahidi kutoa mifuko 100 ya simenti huku diwani wa kata ya kifanya Nolasco Mtewele akiahidi Kuchangia mifuko mifuko 50 ya saruji kumuunga mkono Rais Magufuli katika kukamilisha ujenzi huo.
Awali Mbunge wa Njombe mjini Edward mwalongo alisema kuwa wananchi hao kwa kushirikiana na halmashauri walijitahidi kuchangia kituo hicho cha afya lakini bado hakijakamilika
"Mh Rais wananchi hawa kwa kushirikiana na halmashauri wamejitahidi sana kuchangia kituo cha afya na kituo chao kinatumika lakini hakijakamilika,wamejenga jengo la upasuaji limeshaezekwa ndio tunaendelea nalo,wamechanga milioni 30 na halmashauri kwa mapato ya ndani wamechangia milioni 30" alisema Mwalongo
Social Plugin