RAIS MAGUFULI ATOA POLE KWA MBUNGE WA IRINGA MJINI MCHUNGAJI PETER MSIGWA ALIYEFIWA NA DADA YAKE JIJINI DAR ES SALAAM


Rais Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli wametoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu na kutoa mkono wa pole kwa familia ya Mbunge wa Iringa Mjini Mch Peter Msigwa ambaye amefiwa na Dada yake Tryphosa Simon Sanga aliyefariki dunia tarehe 30 Machi, 2019 kwa ajali ya gari Jijini Dar es Salaam.

Wakiwa nyumbani kwa Marehemu Kimara Stopover, Jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli na Mama Janeth Magufuli wameungana na wanafamilia kumuombea Marehemu apumzike mahali pema peponi, Amina.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم