Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Reuters, Rais wa Sudan Omar Al-Bashir tayari ameshaachia ngazi na makubaliano juu ya kuundwa kwa serikali mpya yanafanyika.
Baadhi ya viongozi wa juu wa serikali akiwemo Waziri wa zamani wa ulinzi na kiongozi wa juu wa chama tawala wanashikiliwa na jeshi.
Tangu asubuhi ya leo, wanajeshi walikuwa wametanda katika makazi rasmi ya rais Omar Al-Bashir na kuzingira njia zote muhimu za kuingia na kutoka mji mkuu wa Khartoum na uwanja wa ndege Khartoum umefungwa.
Social Plugin