Mohamed Salah akishangilia na Andy Robertson (kulia) baada ya kuifungia Liverpool bao la pili dakika ya 80 katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Southampton usiku wa Ijumaa kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa St Mary's.
Mabao mengine ya Liverpool yamefungwa na Naby Keita dakika ya 36 na Jordan Henderson dakika ya 86 wakati la Southampton limefungwa na Shane Long dakika ya tisa na kwa ushindi huo Wekundu hao wa Anfield wanafikisha pointi 82 katika mchezo wa 33 na kurejea kileleni mwa Ligi Kuu, sasa wakiizidi pointi mbili Manchester City ambao hata hivyo ina mchezo mmohja mkononi PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Social Plugin