Akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya, Sophia Mwakagenda, Naibu Waziri wa Kilimo, Innocent Bashungwa bungeni leo Aprili 30, amesema mkakati wa Serikali ni kutafuta wanunuzi wakubwa duniani kununua mazao kwenye mnada huo na kuachana na ule wa Mombasa nchini Kenya.
Awali Bashungwa pia ametoa onyo kwa baadhi ya wafanyabiashara wa pamba ambao wameanza kununua zao hilo kabla ya msimu kuanza Mei mwaka huu.
Akijibu swali la Mbunge wa Sumve, Richard Ndassa kuhusu nini kauli ya Serikali kwa wafanyabiashara walioanza kununua pamba kwa Sh 600 na 700.
Bashungwa amesema: “Anayenunua pamba kabla ya msimu kuanza rasmi ni kosa kisheria na atawasiliana na Wakuu wa Mikoa washughulikie suala hilo,”.
Social Plugin