Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SERIKALI KULETA MABEHEWA NA VICHWA VYA TRENI YA UMEME 1,400

Msemaji wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas amebainisha kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa Serikali inatarajia kuleta mabehewa na vichwa vya treni ya umeme 1,400.


Hayo yamebainishwa alipokuwa akizungumzia tukio la uungwaji wa reli ya treni za Umeme, Standard Gauge Railway kuunganishwa kwa vipande vya SGR na kufanya reli hiyo kuwa moja kutoka Morogoro hadi Dar uliofanyika Aprili 14, 2019 katika kijiji cha Soga mkoani Pwani na kuhudhuriwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isaack Kamwelwe

Waziri Kamwele alieleza kuwa ifikapo mwezi wa saba mwaka huu, Mkandarasi wa reli hiyo ya Shirika la Reli nchini(TRC) wataleta kichwa cha treni ya umeme kwa ajili ya majaribio kwenye kipande cha reli cha Kilometa 30.

Mradi mkubwa wa ujenzi wa reli ya kisasa ya Standard Gauge – unaendelea. Reli hiyo itaanzia bandari ya Dar es Salaam hadi mji mkuu wa Dodoma na baadaye hadi nchi za jirani za Rwanda Burundi na DR Congo.

==>>Tazama hapo chini


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com