Sokwe wawili hawakutaka kupitwa na msisimuko wa picha baada ya afisa wa kupambana na biashara haramu dhidi ya wanyama pori kuchukua simu yake na kuchukua picha nao mnamo Alhamisi, Aprili 18,2019.
Sokwe hao, Ndakasi na Matabishi wanaishi katika mbuga ya wanyama ya Virunga katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na ambayo inalindwa na maafisa 600 wa wanyama pori.
Afisa huyo Patrick Sadiki, alikuwa akipiga doria kama ilivyo ada wakati aliichukua simu yake akinuia kupiga picha wakati sokwe hao walisimama nyuma yake na kuachilia pozi ili wasipitwe na uhondo.
Mbuga hiyo iliyoanzishwa mwaka wa 1925 ni baadhi ya maeneo yaliyo na usalama wa hali ya juu.
Ndani ya mbuga hiyo ya wanyama ambayo ina mazingira ya kuvutia ni makao ya sokwe wa milimani ambao wameorodheshwa kama viumbe ambao maisha yao yamo hatarini.