Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amefafanua sababu ya kuwazuia waandishi wa habari kufanya mahojiano na wabunge wa upinzani kwa kusema wabunge hao wamekuwa na utaratibu wa kutoka nje mara kwa mara.
Spika Ndugai ametoa ufafanuzi huo jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya kauli yake aliyoitoa ya kuwazuia waandishi wa habari kufanya mahojiano na wabunge wa upinzani ambao waliamua kutoka nje ya Bunge baada Mbunge Arusha Mjini kusimamishwa mikutano 3 ya Bunge.
"Hatukusema sasa waandishi msiwe mnaongea na wabunge huko nje, lakini waandishi mkiacha kuwafuatilia wataacha wakitoka saa saba si Bunge limeahirishwa wakasema wanayotaka, wakitoka wanaleta mtafaruku na kusababisha mijadala muhimu ya ndani ya Bunge isiwe na waandishi." amesema Spika Ndugai
Kuhusiana na hatma ya Mbunge Lema, Spika Ndugai amesema, "kuna watu wana madeni makubwa zaidi ya hayo lakini hayawachanganyi, na sisi Bunge next time niwepo au nisiwepo tutawalisisha watakaokuwepo tusiruhusu tena Bunge kudhamini wabunge kuingia kwenye madeni makubwa".
"Wanaotetea lazima watetee kwa sababu hawajui hali halisi ni nini, lakini mwisho wa siku hela yenu ndiyo inayotumika wale waliotimuliwa nane (wabunge wa CUF) inadaiwa zaidi ya bilioni 1 na hawana uwezo wowote wa kulipa, kama watakazia wale jamaa na kuna some how kodi yenu inaweza kutumika" amesema Spika Ndugai
Social Plugin