Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Spika wa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai ameishauri Serikali kuwa na mpango wa kutoa kipaumbele cha kwanza katika kuajiri walimu wa Masomo ya Sayansi ili kupunguza uhaba wa walimu hao hapa nchini.
Mhe.Ndugai ameyasema hayo leo bungeni jijini Dodoma wakati akitoa mchango wa nyongeza baada ya Mbunge wa Buhigwe Mhe.Albert Obama aliyehoji mpango wa Serikali kuongeza walimu wa Masomo ya Sayansi.
Mhe.Ndugai katika Msisitizo wake amesema kuna baadhi ya shule katika jimbo lake unakuta kuna mwalimu mmoja tu wa Masomo ya Sayansi hususan somo la hesabu hivyo kuna haja ya serikali katika awamu nyingine ya ajira ikaajiri walimu pekee wa Masomo ya Sayansi hata kama ni elfu nne huku Mbunge wa Buhigwe Alrbert Obama Ntabaliba akihoji pia juu ya kuongeza vifaa vya Maabara.
Akijibu Maswali hayo,Naibu Waziri wa nchi,Ofisi ya Rais na Serikali za Mitaa Mwita Waitara amesema serikali inafanya mchakato wa kuajiri zaidi ya walimu elfu nne kwa kuzingatia maeneo yenye upungufu zaidi na awamu ya pili ya kutoa ajira serikali itazingatia maeneo yenye mapungufu zaidi walimu wa Masomo ya Sayansi.
Hata hivyo Naibu Waziri,Waitara amesema kwa mwaka wa fedha 2018/2019 serikali inatarajia kununua na kusambaza vifaa vya Maabara katika shule za sekondari 1250 zilizokamilisha vyumba vya maabara hapa nchini.
Social Plugin