Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi amesema yeye ni miongoni mwa Wabunge ambao wanamuunga mkono Rais Magufuli licha ya kutohama chama na amedai ataendelea kumuunga mkono hadi mwisho.
Mbunge Sugu ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Ruanda, Nzovwe jijini Mbeya leo Aprili 26, 2019.
"Mimi ni katika watu tunaokuunga mkono bila kuhama chama, na nitaendelea kukuunga mkono mpaka mwisho, wanasema kuna watu wamepanga kufanya fujo, haiwezekani watu na akili zao wapange kumfanyia fujo Rais," amesema Mbunge Sugu.
Akizungumzia changamoto ya maji katika jiji la Mbeya, Mbunge huyo alisema Sh70 bilioni zinahitajika ili kumaliza tatizo la maji huku chanzo chake ikiwa ni Mto Kiwila.
Amesema kwa mujibu wa wataalamu njia hiyo itakuwa ni tiba ya shida ya maji katika jiji la Mbeya na hata mkoa jirani wa Songwe.
Social Plugin