Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini Tanzania (TMA) imetoa taarifa mpya juu ya mwenendo wa kimbunga Kenneth na kusema kuwa kinatarajiwa kutua kesho Ijumaa alfajiri au asubuhi.
Katika Taarifa ya video iliyopakiwa kwenye mtandao wa kijamii wa You Tube, Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt Agness Kijazi amesema kufikia saa tia mchana wa leo kimbunga kitakuwa umbali wa kilomita 177 kutoka pwani ya Mtwara kikiwa na kasi ya kilometa 140 kwa saa.
Kutokana na kasi hiyo kimbunga kinatarajiwa kutua nchini Msumbiji kuanzia Alfajiri ya Ijumaa kikiwa na kasi kilomita 100 kwa saa.
Hata hivyo, kitakapotua kimbunga hicho ni karibu na mpaka wa Tanzania kwa kilomita 230, na athari zake zinatarajiwa kukumba maeneo yaliyo ndani ya kilomita 600.
"Nchini mwetu, maeneo ya mpaka Lindi na Ruvuma yataathirika sana," amesema Kijazi na kuongeza, "wakazi hususani wa Mtwara kwa sasa wanaweza wakaona tu kuna mvua zinanyesha lakini waendelee kuchukua tahadhari. Kadri muda unavyosidi kusonga ndiyo kimbunga kinazidi kukaribia nchi kavu."
==>>Msikilize hapo chini
Social Plugin