Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TAHADHARI YA KIMBUNGA YATOLEWA MTWARA...WAFANYAKAZI NA WANAFUNZI WAAGIZWA KUSALIA MAJUMBANI


Na Bakari Chijumba, Mtwara.
Kufuatia Mamlaka ya Hali ya hewa Tanzania(TMA),kutoa angalizo la uwezekano wa kutokea Kimbunga katika  pwani ya kusini mwa Tanzania kesho Alhamisi  25/04/2019, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa ameagiza watumishi wote wasiende makazini kesho,pia wanafunzi ngazi zote wasiende mashuleni na vyuoni.


Bakyanwa amesema taarifa zinaonesha kuanzia asubuhi saa mbili hadi tatu zitaanza mvua za kawaida,ila baadae utafuata upepo mkali,radi na mvua kubwa zinazoweza sababisha Mafuriko na kimbunga na kwamba  licha ya kwamba ni utabiri lazima tahadhari ichukuliwe.

"Tumepata angalizo la kutokea Kimbunga..Kamati ya usalama wa mkoa tumekubaliana,kesho watu wote wanaoishi mabondeni watoke na wakae sehemu zenye miinuko,Pia watu wasiende makazini,mashuleni wala Vyuoni,kwa ajili ya kuangalia hali itakavyokuwa" amesema Byakanwa na kuongeza kwamba;

"Tumepata angalizo la kutokea Kimbunga..Kamati ya usalama wa mkoa tumekubaliana,kesho watu wote wanaoishi mabondeni watoke na wakae sehemu zenye miinuko,Pia watu wasiende makazini,mashuleni wala Vyuoni,kwa ajili ya kuangalia hali itakavyokuwa"

Kwa upande wake Ofisi ya Mkurugenzi Manispaa ya Mtwara Mikindani imewataka wananchi wanaoishi maeneo hatarishi kama Chuno,Miseti,Skoya,Reli,Kiyangu,kiyangu,Mtepwezi,Mikindani &maeneo yaliyopo pembezoni mwa Bahari kuondoka na kwenda kujihifadhi katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kujihifadhi.

"Wananchi wametakiwa kuwa na Akiba ya Chakula cha kutosha siku ya Kesho Maeneo yaliyotengwa ili kujihifadhi ni shule ya msingi Majengo,Shule ya Msingi Tandika,Sekondari ya sabasaba,uwanja wa ndege,Naliendele Jeshini na Mitengo  na Sabodo Secondary" imesema taarifa hiyo kutoka ofisi ya Mkurugenzi.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com