Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Dodoma imesema inachunguza ufisadi wa shilingi Milioni 900 baada ya kuwa na viashiria vya rushwa katika miradi mbalimbali.
Pia taasisi hiyo imefanikiwa kuokoa kiasi cha Sh152.3 milioni ambazo zingelipwa kwa wakandarasi ambao ufuatiliaji wa ukaguzi wa miradi ya maji umebaini hawakutimiza majukumu yao ipasavyo.
Hayo yamebainishwa jana mkoani Dodoma na kamanda wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU, mkoa wa Dodoma Sosteth kibwengo wakati akitoa taarifa ya robo ya mwaka kwa wanahabari.
Ambapo alisema kwa robo ya mwaka taasisi hiyo imefanikiwa kuokoa zaidi ya shilingi milioni 152.3, zilizokuwa zilipwe kwa wakandarasi ambao hawakutekeleza majukumu yao kikamilifu.
Taasisi hiyo pia imemtaka mkurugenzi wa kampuni ya Global Space East Africa Limited, inayojenga kituo cha afya Mima kilichopo Wilayani Mpwapwa mkoani hapa kulipoti katika ofisi ya zake zilizopo wilayani humo kwa mahojiano.
Vile vile alibainisha kuwa katika kipindi husika, TAKUKURU ilipokea jumla ya taarifa 96 za rushwa na makosa yahusianayo ambapo sekta ziliongoza kwa tuhuma ni;
Serikali za mitaa (25%), Ardhi (17%), Elimu (16%), Afya (8%), Maji, Ujenzi na Mahakama (kila moja asilimia 7), na Polisi (6%), taarifa hizo zilifanyiwa kazi kwa njia mbalimbali na majalada nane (8) ya uchunguzi yalikamilika ikiwa ni ongezeko la asilimia 12.5 ya majalada yaliyokamilika kwa kipindi hicho mwaka 2018.
Social Plugin