Mfanyabiashara, Florencia Mashauri ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Zenon Oil and Gas Limited amefikishwa Mahakamani leo na TAKUKURU kwa kujibu mashtaka ya wizi, uhujumu uchumi, ukiukwaji wa sheria ya mafuta juu ya ujengaji wa kituo cha uuzaji wa mafuta kwa UDART pamoja na makosa ya utakatishaji wa fedha haramu ya zaidi ya shilingi Bilioni 1.2.
Mashauri ni mke wa mfanyabiashara Robert Kisena ambaye naye ana kesi ya uhujumu uchumi.
Kaimu Mkurugenzi wa Uchunguzi Takukuru, Kassim Ephrahim amewaeleza waandishi wa habari leo Aprili 10, 2019 kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa jana.
Amesema katika uchunguzi wa Takukuru imebainika kuwa licha ya kampuni hiyo kusajiliwa kuingiza mafuta kwa wingi, haikuwahi kuagiza mafuta hayo na badala yake ilikuwa ikijihusisha na uuzaji wa petroli na dizeli kwa rejareja kwa kampuni ya Udart.
Social Plugin