Timu ya Simba imetoka suluhu ya bila kufungana dhidi ya TP Mazembe leo Jumamosi mchezo wa Ligi ya Mabingwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Simba na Mazembe zimecheza mchezo wao wa kwanza wa robo fainali ya Klabu Bingwa Afrika na watarudiana Aprili 13 nchini Congo, Lubumbashi.
Katika mchezo huo wote walikuwa wanacheza kwa kuviziana katika kutafuta bao. Hata hivyo Mazembe walikuwa wakishambulia mara kwa mara goli la Simba lakini utulivu wao ulionekana kuwa mdogo katika kuhakikisha wanapata goli la kuongoza.
Kwa upande wa Simba walikuwa wanamtegemea zaidi Meddie Kagere kuwatanguliza mbele hata hivyo naye alikuwa anakutana na ubabe kutoka kwa mabeki wa Mazembe.
Dakika 30 Kagere alitaka kuifungia goli la kuongoza Simba baada ya kubinuka Tiktaka akipokea krosi ya Zana Coulibally na mpira kugonga mwamba kisha ukaambaa na mabeki wa Mazembe kuuondoa haraka.
Na Thomas Ng'itu
Social Plugin