Mkuu wa Kitengo cha Elimu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bi Faith Shayo akitambulisha meza kuu wakati wa hafla fupi ya Unesco kukabidhi Tanzania mradi wa kutumia Tehama kujifunza na kufundisha masomo ya sayansi, hisabati na lugha kwa ufadhili wa China iliyofanyika Chuo cha Ualimu Monduli jijini Arusha.
Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bw. Tirso Dos Santos (wa tatu kushoto) akitoa salamu za Unesco kwa wageni waalikwa (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya Unesco kukabidhi Tanzania mradi wa kutumia Tehama kujifunza na kufundisha masomo ya sayansi, hisabati na lugha kwa ufadhili wa China iliyofanyika Chuo cha Ualimu Monduli jijini Arusha.
Mwakilishi wa Balozi wa China nchini, Zhang Bin (kushoto) akitoa salamu za Jamhuri ya watu wa China kwa wageni waalikwa (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya Unesco kukabidhi Tanzania mradi wa kutumia Tehama kujifunza na kufundisha masomo ya sayansi, hisabati na lugha kwa ufadhili wa China iliyofanyika Chuo cha Ualimu Monduli jijini Arusha.
Kamishina wa Elimu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Dk Lyabwene Mutahabwa (wa tatu kulia) akizungumza kwa niaba ya Naibu katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi (MoEVT), Dr. Ave Maria Semakafu wakati wa hafla fupi ya Unesco kukabidhi Tanzania mradi wa kutumia Tehama kujifunza na kufundisha masomo ya sayansi, hisabati na lugha kwa ufadhili wa China iliyofanyika Chuo cha Ualimu Monduli jijini Arusha.
Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bw. Tirso Dos Santos (katikati) akimkabidhi Kamishina wa Elimu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Dk Lyabwene Mutahabwa ( wa tatu kulia) nyaraka zinazohusu mradi wa kufundisha kwa Tehama katika hafla fupi iliyofanyika Chuo cha Ualimu Monduli jijini Arusha. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mwakilishi wa Balozi wa China nchini, Zhang Bin (wa tatu kushoto), Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Unesco, Dr. Hamisi Malebo (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Kitengo cha Elimu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi,Bi. Augusta Lupokela (wa pili kulia), Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu nchini Dr.Aneth Komba (kushoto) pamoja na Kiongozi wa Timu ya Kitaifa ya Usimamizi wa Mradi, Prof. Ralph Masenge (kulia).
Kamishina wa Elimu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Dk Lyabwene Mutahabwa ( wa tatu kulia) akikata utepe mara baada ya kupokea nyaraka zinazohusu mradi wa kutumia Tehama kujifunza na kufundisha masomo ya sayansi, hisabati na lugha kwa lengo la kuinua kiwango cha elimu nchini uliofadhiliwa na China na kuratibiwa na Unesco kwenye hafla iliyofanyika Chuo cha Ualimu Monduli jijini Arusha. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bw. Tirso Dos Santos (katikati), Mwakilishi wa Balozi wa China nchini, Zhang Bin (wa tatu kushoto), Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Unesco, Dr. Hamisi Malebo (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Kitengo cha Elimu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Bi. Augusta Lupokela (wa pili kulia), ), Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu nchini Dr.Aneth Komba (kushoto)pamoja na Kiongozi wa Timu ya Kitaifa ya Usimamizi wa Mradi, Prof. Ralph Masenge (kulia).
Kamishina wa Elimu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Dk Lyabwene Mutahabwa ( wa tatu kulia) akionyesha nyaraka zinazohusu mradi wa kutumia Tehama kujifunza na kufundisha masomo ya sayansi, hisabati na lugha kwa lengo la kuinua kiwango cha elimu nchini uliofadhiliwa na China na kuratibiwa na Unesco kwenye hafla iliyofanyika Chuo cha Ualimu Monduli jijini Arusha. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bw. Tirso Dos Santos (katikati), Mwakilishi wa Balozi wa China nchini, Zhang Bin (wa tatu kushoto), Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Unesco, Dr. Hamisi Malebo (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Kitengo cha Elimu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Bi. Augusta Lupokela (wa pili kulia), Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu nchini Dr.Aneth Komba (kushoto) pamoja na Kiongozi wa Timu ya Kitaifa ya Usimamizi wa Mradi, Prof. Ralph Masenge (kulia).
Mratibu wa Miradi wa Taifa wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi Regina Monyemangene akiwasilisha mada inayohusu mafanikio na uendelevu wa mradi wa CFIT wakati wa hafla fupi ya Unesco kukabidhi Tanzania mradi wa kutumia Tehama kujifunza na kufundisha masomo ya sayansi, hisabati na lugha kwa lengo la kuinua kiwango cha elimu nchini uliofadhiliwa na China na kuratibiwa na Unesco kwenye sherehe iliyofanyika Chuo cha Ualimu Monduli jijini Arusha. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Elimu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bi Faith Shayo.
Kiongozi wa Timu ya Kitaifa ya Usimamizi wa Mradi, Prof. Ralph Masenge akitoa neno la shukrani kwa niaba ya timu nzima iliyoshiriki mradi wa CFIT wakati wa hafla fupi ya Unesco kukabidhi Tanzania mradi wa kutumia Tehama kujifunza na kufundisha masomo ya sayansi, hisabati na lugha kwa lengo la kuinua kiwango cha elimu nchini uliofadhiliwa na China na kuratibiwa na Unesco katika sherehe iliyofanyika Chuo cha Ualimu Monduli jijini Arusha.
Mwakilishi wa wanafunzi wa Chuo cha Ualimu Monduli, Okumu Peter akitoa neno la shukrani wakati wa hafla fupi ya Unesco kukabidhi Tanzania mradi wa kutumia Tehama kujifunza na kufundisha masomo ya sayansi, hisabati na lugha kwa lengo la kuinua kiwango cha elimu nchini uliofadhiliwa na China na kuratibiwa na Unesco katika sherehe iliyofanyika Chuo cha Ualimu Monduli jijini Arusha.
Baadhi ya viongozi wa MoEVT, Unesco, Ubalozi wa China na Vyuo vinavyonufaika na mradi wa CFIT wakiwa kwenye ziara kuangalia mradi wa CFIT unavyotekelezwa katika Chuo cha Ualimu Monduli kilichopo jijini Arusha.
Mmoja wa wanafunzi wa Chuo cha Ualimu Monduli akiwa kwenye mafunzo ya Tehama chuoni hapo wakati wa ziara kuangalia mradi wa CFIT unavyotekelezwa katika chuo hicho kilichopo jijini Arusha ambapo kumefanyika hafla ya Unesco kukabidhi Tanzania mradi wa kutumia Tehama kujifunza na kufundisha masomo ya sayansi, hisabati na lugha kwa lengo la kuinua kiwango cha elimu nchini uliofadhiliwa na China.
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla fupi ya Unesco kukabidhi Tanzania mradi wa kutumia Tehama kujifunza na kufundisha masomo ya sayansi, hisabati na lugha kwa lengo la kuinua kiwango cha elimu nchini uliofadhiliwa na China na kuratibiwa na Unesco katika sherehe iliyofanyika Chuo cha Ualimu Monduli jijini Arusha.
Kamishina wa Elimu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Dk Lyabwene Mutahabwa katika picha ya pamoja na viongozi wa UNESCO, MoEVT, Ubalozi wa China pamoja na Viongozi wa vyuo vilivyonufaika na mradi wa CFIT mara baada ya kupokea rasmi mradi huo kutoka Unesco uliofadhiliwa na China.
***
SERIKALI ya Tanzania imeshukuru mchango wa Jamhuri ya watu wa China katika kufanikisha programu yake ya kuboresha taaluma nchini kwa kunoa walimu wanaoweza kutumia Tehama kujifunza na kufundisha masomo ya sayansi, hisabati na lugha.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi (MoEVT), Dr. Ave Maria Semakafu.
Katika hotuba iliyosomwa kwa niaba na Kamishina wa Elimu, Dk Lyabwene Mutahabwa wakati wa kukabidhiwa awamu ya pili ya mradi wa kuboresha elimu (CFIT ) kwa ufadhili wa China, hafla iliyofanyika Chuo cha Elimu Monduli jana.
Naibu Katibu mkuu huyo alisema kwamba kumekuwepo na mafanikio makubwa ya kujivunia katika mradi huo na ni mategemeo yake kwamba China itaendelea kusaidia katika awamu nyingine zijazo.
Amesema serikali inatambua kuwa rafiki wa kweli ni yule anayekusaidia kunoa wananchi wako, kwani kupitia elimu ndiko mabadiliko ya kiuchumi yanapowezekana.
Alisema kutokana na ukweli huo Tanzania inathamini ushirikiano wake na China, ushirikiano ambao inaamini utaendelea kujengwa kwa manufaa ya pande zote mbili.
“Huyu ni rafiki wa kweli anatusaidia kuwa wabobezi katika sayansi na teknolojia, bila kuwa na walimu wazuri wa kuendeleza sayansi, hesabu na teknolojia taifa haliwezi kuendelea” alisema Ave Maria kupitia Kamishina huyo wa elimu.
Alisema kwa kuwanoa walimu, watakuwa wamewezesha taifa kuzalisha wanafunzi bora ambao watakuwa na uelekeo wenye weledi wa kutosha kujumuika katika kujenga uchumi wa nchi.
Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa kushirikiana na MoEVT chini ya ufadhili wa Serikali ya China (UNESCO-China Funds-in-Trust -CFIT) umekuwa ukitekeleza mradi wa kuboresha uwezo wa walimu katika masomo ya sayansi kwa lengo la kuinua kiwango cha elimu nchini.
Mradi huo unaoendeshwa na serikali ya Tanzania na UNESCO ulitiwa saini Mei 7,2015 na kushuhudiwa na Balozi wa China Tanzania, Dk. Lu Youqing.
Mradi huo ulioanza mwaka 2017 umelenga kuboresha uwezo wa walimu katika vyuo viwili vya walimu vinavyofunza masomo ya sayansi na hesabu vya Monduli na Tabora.
Katika mafunzo hayo walimu walikuwa wakipatiwa mafunzo ya Tehama kwa lengo la kuwaptia weledi wa kutumia mafunzo hayo kwa kufundisha na pia kujifunza.
Katika programu hiyo, vyuo hivyo vimewezeshwa kushirikiana kielimu na vyuo vingine vinane vya ualimu vinavyofunza masomo ya sayansi na hesabu.
Vyuo vya Tabora na Monduli vitawezesha maandalizi ya programu za sayansi na hesabu zitakazotumika kufunza walimu wengine kupitia Tehama na kuimarisha programu mbalimbali za ubunifu kwa kufundisha kwa tehama.
Tanzania ni miongoni mwa mataifa ambayo yametambua matumizi ya Tehama katika kuimarisha elimu na kusaidia kusukuma mbele uchumi na kuwa miongoni mwa nchi nane zinazopatiwa msaada huo kwa ufadhili wa China.
Mradi huo umeeleza kuchangia juhudi za serikali katika kukabiliana na changamoto mbalimbali ili kuwezesha elimu bora.
Taasisi kadhaa zinahusika na mradi huo zikiwamo Chuo Kikuu Huria (OUT) na Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE).
Awamu ya pili ya mradi wa UNESCO-CFIT ni sehemu ya mradi mkubwa unaodhaminiwa na China ambao umelenga kupunguza pengo la ubora wa elimu katika bara la Afrika.
Mradi huo ulizinduliwa machi 2017 nchini Ethiopia.
Awamu ya pili imejengwa katika mafanikio ya awamu ya kwanza.
Awamu ya kwanza ilizinduliwa mwaka 2012 kwa msaada wa Serikali ya China iliyotoa bajeti ya dola za Marekani milioni 8 kwa kipindi cha miaka minne.
Nchi nane zinashiriki katika mradi huo ambazo ni Côte d’Ivoire, Ethiopia, Namibia (zilizofanya 2012 – 2015), Congo, DR Congo, Liberia, Tanzania na Uganda (zilizofanya 2013 –2016).
Naye mwakilishi wa Balozi wa China nchini, Zhang Bin amesema kwamba taifa lake litaendelea kushirikiana na Unesco na Tanzania katika kufanikisha programu za elimu.
Alisema nchi yake inaamini kwamba elimu ni kichocheo cha maendeleo na kwamba katika miaka 55 ya uhusiano na Tanzania, imekuwa ikishirikiana nayo katika nyanja mbalimbali.
Katika ushirikiano huo pia amesema Tanzania imepatiwa walimu zaidi ya 100 kwa lengo la kufundisha lugha na utamaduni wa China kwa wanafunzi 17,000 wanaotaka kujifunza masuala ya China kupitia taasisi ya Confucius, kama sehemu ya kujiimarisha kifikira na kiuchumi.
Wakati huo huo Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bw. Tirso Dos Santos amesema kwamba shirika lake limefurahishwa jinsi mradi huo ulivyotekelezwa na kwamba ni sehemu ya juhudi kubwa ya shirika lake katika kuteleleza malengo ya maendeleo endelevu ya dunia katika elimu.
Alisema katika hilo hakuna mtu aliyepaswa kuachwa nyuma na kwamba ni lengo lake kuongeza ubora wa elimu na matumizi ya teknolojia ya kisasa kufikisha elimu kwa wote.
Katika makabidhiano hayo pamoja na kuipongeza serikali na wizara ya elimu pia alizipongeza taasisi mbalimbali zilizohusika katika kuhakikisha kwamba mradi unafanikiwa hasa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).
Pia alishukuru serikali ya China na Tanzania kwa kufanikisha mradi huo ambao pamoja na mambo mengine uliwezesha kuwapo kwa miundombinu ya kufundisha kwa njia ya Tehama na pia kutengeneza ubunifu unaostahili wa kufundisha masomo ya sayansi kwa Tehama na kutengeneza maktaba kubwa ya elimu ya Tehama.
Social Plugin