Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha (RTO) Joseph Bukombe akizungumza na madereva wa magari ya abairia, binafsi na madereva bodaboda katika uzinduzi wa kampeni ya kunywa kistaarabu iliyozinduliwa leo jijini Arusha.
Mkurugenzi wa Uhusiano wa SBL, John Wanyancha akizungumzia kampeni ya kunywa kistaarabu maarufu kama ‘Usinywe na Kuendesha Chombo cha Moto’
Mkurugenzi wa Uhusiano wa SBL, John Wanyancha akizungumza na madereva bodaboda katika stendi kuu ya mabasi Jijini Arusha.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha (RTO) Joseph Bukombe akimvisha kizibao cha kisibqo chakung'aa mmoja wa madereva bodaboda katika stendi kuu ya mabasi jijini Arusha.
Mwenyekiti wa mabalozi wa usalama barabarani Bakari Msangi akimvisha mmoja wa dereva bodaboda kizibao cha kung'aa (reflector) katika kampeni iliyozinduliwa Jijini Arusha ya kunywa kistaarabu na kampuni ya Serengeti.
Mwenyekiti wa bodaboda akizungumza katika uzinduzi wa kampeni hiyo ya kunywa kistaarabu stendi kuu ya mabasi Jijini Arusha. Picha na Vero Ignatus.
Na. Vero Ignatus, Arusha
Madereva wa vyombo vya moto Mkoani Arusha watakiwa kutotumia vilevi wakati wawapo barabarani
Arusha, Aprili 5, 2019 : Kampeni ya unywaji wa kistarabu inayoendeshwa na Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) imezinduliwa rasmi Mkoani Arusha ambapo madereva wa vyombo vya moto wametakiwa kuzingatia sheria za barabarani na kutotumia vilevi wakati wa kazi.
Kampeni hiyo maarufu kama ‘Usinywe na Kuendesha Chombo cha Moto’ imeenda sambamba na ugawaji wa makoti ya usalama (Reflectors) kwa madereva bodaboda mkoani humo ikiwa ni mkakati wa kuhimiza matumizi ya vifaa hivyo kwa usalama wa watumiaji wa barabara.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika leo katika Makao Makuu ya Traffic jijini hapa, Mkurugenzi wa Uhusiano wa SBL, John Wanyancha amesema kampeni hiyo imelenga kutoa elimu kwa wateja wake nchini ili kupunguza matukio yanayoepukika kama ajali zitokanazo na unywaji wa pombe kupindukia.
“Pombe isipotumika kiistarabu inaweza kuleta madhara katika jamii na mojawapo ya madhara ni pale mtu anapokunywa pombe na akaendesha chombo cha moto ikasababisha ajali jambo ambalo ni hatari kwa madereva na pia ni hasara kwa Taifa,” alisema
Kampeni hiyo inashirikisha wadau mbalimbali ikiwamo Jeshi la Polisi-Kikosi cha usalama barabarani, Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), madereva bodaboda pamoja na jamii kwa ujumla ikilenga katika kupunguza ajali zitokanazo na ulevi wa kupindukia nchini.
Kwa upande wake,Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha (RTO) Joseph Bukombe alisema kampeni hiyo itasaidia katika kupunguza ajali zinazosababishwa na ulevi huku akiwataka madereva kuzingatia kuacha kutumia vilevi ili kujihakikishia usalama wawapo barabarani.
Madereva bodaboda atakayekamatwa anaendesha hana leseni pikipiki itazuiliwa atalipia shilingi 25,000 ataingia darasani kusoma akimaliza kusoma atapewa cheti chake halafu anaanza kushughulikia leseni yake. Alisema RTO.
“Unywaji wa pombe kiistarabu ni suala la muhimu sana kwa madereva kwasababu madereva wakiwa kwenye hali ya ulevi ni moja ya chanzo cha ajali za barabarani hivyo tunaipa kipaumbele kampeni hii hapa mkoani Arusha na tutaendelea kutilia mkazo suala hili,” alisema
Bukombe amewakumbusha madereva na wamiliki wa vyombo vya usafiri kuwa Stika za usalama barabarani zimeshatoka hivyo wapeleke pikipiki zao kukaguliwa kwa shilinhi 1000,magari ya watu binafsi 3000,magari ya biashara 5000
Aliipongeza SBL kwa kuona umuhimu wa kuwalinda watumiaji wa barabara kwa kutoa elimu hiyo kwa madereva na umma kwa ujumla. “Pamoja na kuwa wao (Serengeti) ni watengenezaji wa pombe lakini wameona wajibu wao wa kumlinda na kuleta usalama wa madereva na watumiaji wengine wa barabara,” alisema
Kwa upande wake mwenyekiti wa mabalozi wa usalama barabarani (RSA) Bakari Msangi amewataka madereva waendesha bodaboda na magari ya Abiria kuwa makini wawapo barabarani na wafuate sheria kama inavyotakiwa
Tunachowasii na kusisitiza ni kutii sheria mnapokuwa kwenye vyombo vya moto, wacheni ulevi mkiwa kazini, kunywa wakati umeshamaliza kazi, tuhqkikishe tunaondoa ajali zote zinazo epukika
Social Plugin